TPHA yawakutanisha wadau wa afya kujadili njia za kutumia kutengeneza sera ya kupunguza unywaji wa pombe

254
0
Share:

dsc_0700Dk. Faustine Njau kutoka Chama cha Afya ya Jamii (TPHA) akifungua mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa Afya ya Jamii ili kujadili ni kwa jinsi gani wanaweza kuunganisha nguvu katika kupinga matumizi ya pombe katika familia hivi karibuni jijini Dar es Salaam. (Picha na Geofrey Adroph).Wadau wa Afya ya Jamii wakiwa wamesimama kumuombea aliyekuwa Mratibu wa Mradi wa Madhara ya Tumbaku (TPHA) Dk. Bertha T.A. Maegga aliyefariki dunia.Mjumbe wa Chama cha Afya ya Jamii (TPHA), Dk. Mashombo Mkamba akizungumzia historia ya Chama cha Afya ya Jamii (TPHA) kwenye semina ya wadau mbalimbali wa wanaopigania matumizi ya pombe katika jamii mbalimbali hapa nchini Tanzania.Mathias Kimilo kutoka Mtandao wa kudhibiti madhara ya pombe akizungumzia madhara yanayowakuta watoto na jamii mara baada ya familia kujikita kwenye unywaji wa pombe katika mkutano uliofanyika hivi karibuni ukumbi wa NIMR  jijini Dar es Salaam.Judith Kimaro kutoka Manispaa ya Kinondoni akizungumzia kesi wanazozipokewa kwa siku kutokana na kuvunjika kwa ndoa ikiwa kisababishi kikubwa ni pombe.Janeth Mawinza kutoka WAJIKI akizungumzia  jinsi familia zinavyoathiriwa na vitendo vya kijinsia vinavyosababishwa na matumizi mabaya ya pombe pamoja na nyingine kutengana kutokana na matumizi ya pombe kwa wazazi wao.Baadhi ya wadau wa Afya wakichangia madaPichani juu na chini ni baadhi ya wadau wa afya wakichangia mada.Baadhi ya wadau mbalimbali wakiwa kwenye semina iliyowakutanisha wadau wa Afya ya Jamii  hivi karibunikatika ukumbi wa NIMR jijini Dar es Salaam.Loyce Gondwe kutoka TAMWA akitoa mada kuhusu sheria zinazohusu pombe kwenye mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa Afya hivi karibuni katika ukumbi wa NIMR jijini Dar es Salaam.

Share:

Leave a reply