Trend Solar waboresha maisha kwa wateja wake ndani ya Sabasaba

730
0
Share:

Watanzania wameshahuriwa kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa ya kuboresha maisha  yao kwa kutumia Trend Solar za kisasa zenye ubora wa hali ya juu zilizoboreshwa sambamba na simu ya kisasa ya Smartphone, Solar paneli ya 20W,Chaja aina ya USB, Betri smati ya Sola, Tochi ya kuchaji,Taa 3 aina ya LED na mishikio ambazo unaweza kutumia chumbani, sebureni na nje ya nyumba yako ambapo kwa vyote hivyo vikipatikana kwa jumla ya Tsh. 531,000.

Trend Solar ambao wapo katika mabanda ya Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam wametoa ofa kabambe ya mteja kulipia kidogo kidogo kwa muda wa Mwaka mmoja.

“Boresha maisha kwa kulipia polepole. Kwa kianzio cha Tsh.93,000 tu! Baada ya hapo utachagua muda wa malipo ya aina mbili, kuna malipo ya wiki ambayo unaweza kulipa Tsh.8,423 ( kwa kila wiki) au ukaweza kulipa Tsh.36,500 malipo ya mwezi.  Hivyo jumla ya malipo ya  mwaka mmoja ni Tsh.531,000″. Alieleza Mtendaji Mkuu wa Trend Solar, Irfan Mirza.

Irfan ameongeza kuwa, Trend Solar ni sola za kisasa na zimekidhi viwango hivyo bidhaa hizo ambazo kwa sasa zimetokea kupendwa watu mbalimbali wamejitokeza kuzinunua na kuboresha maisha yao kwa nyumba zao kupata mwangaza wa taa, kupata mawasiliano ya kisasa ya simu ya smati trend solar ambayo inauwezo mkubwa wa kupiga picha, kuchati, kupakua App mbalimbali na mambo mengine.

Trend Solar wapo nje ya banda la Halotel ama jirani na hema la Mikumi ndani ya viwanja hivyo vya Sabasaba. Pia waweza kuwasiliana nao kwa kupiga simu ya bure bila malipo :0800713333 au kutembelea katika ofisi zao zilizopo jingo la RITA Tower 9th Floor lililopo mtaa wa Simu/Makunganya.

Mifumo yote inakuja kwa warantii ya miaka  2 katika betri smati ya sola na vifaa vingine kama vile balbu, simu, sola peneli na vingine vina warantii ya mwaka 1.

Waweza kutembelea mtandao wao kwa taarifa zaidi: http://boreshamaisha.com/

Arfan Mirza na Bi Natalie wakiwa kwenye bango hilo la Trend Solar 

Romanus Haule wa Trend Solar akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) juu ya huduma za bidhaa hizo

Arfan Mirza akijadiliana jambo na wajumbe wa Trend Solar wakati walipotembelea banda hilo

Leahlisa kutoka Trend Solar akitoa maelezo  kwa wateja waliotembelea banda hilo

Marwa kutoka Trend Solar akitoa maelezo kwa wateja walifika kwenye banda hilo

Bi Natalie wa Trend Solar akiwa na mteja aliyenunua Trend Solar kwenye banda hilo mapema leo Julai 7,2017 .

Timu ya Trend Solar wakiwa tayari kutoa huduma ndani ya banda lao kwenye maonyesho ya 41 ya Sabasaba

Share:

Leave a reply