Treni ya abiria ikitokea Kigoma kwenda Dar, yaanguka huko Ruvu Mkoani Pwani

876
0
Share:

Treni ya mwendo haraka, (DELUX), iliyokuwa ikitokea Kigoma  kwenda jijini Dar es Salaam, imeanguka eneo la Ruvu mkoani Pwani jioni hii ya Jumapili Januari 29, 2017.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka eneo la ajali,zinasema takriban mabehewa 10 kati ya 20 yameanguka na juhudi za kuwaokoa watu zilikuwa zikiendelea na watu kadhaa walionekana wakiwa wamelala chini wengine hawajiwezi kabisa.

Msemaji wa TRL, Medladjy Maez amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, na alipoongea na mwandishi wa habari hizi majira ya saa 11;13 jioni, amesema treni hiyo imeanguka na ni mabehewa matano ya abiria yameanguka na moja limeacha njia, lakini hakuwa na taarifa zaidi kwani ndio alikuwa anajiandaa kuelekea eneo la tukio.

“Ni kweli treni yetu ya Delux iliyokuwa ikitokea Kigoma na kutarajiwa kuwasili hapa saa 11:30, imeanguka eneo la Ruvu, na mabehewa matano yameanguka na moja limeacha njia, taarifa zaidi tutazitoa kuhusu walioathirika kwa sasa tunajiandaa kwenda eneo la tukio” Alisema Maez.

Habari na Khalfan Said wa K-VIS BLOG

Treni hiyo iliyoangula..

Treni hiyo iliyoangula..

Share:

Leave a reply