Trilioni 48.2 kutumika kujenga ukuta wa Marekani na Mexico

1008
0
Share:

Mpango wa Rais wa Marekani, Donald Trump kujenga ukuta baina ya taifa hilo na majirani zao Mexico umekadiriwa hadi kukamilika utatumia Dola Bilioni 2.6 ambazo ni sawa na Trilioni 48.2 kwa pesa ya Kitanzania.

Ujenzi wa ukuta huo ambao utakuwa na urefu wa kilomita 2,000 unatarajiwa kujengwa kwa kipindi cha miaka mitatu na nusu na ujenzi wake utamalika mwaka 2020.

Aidha ripoti hiyo inatarajiwa kukabidhiwa kwa Waziri wa Usalama wa Marekani, John Kelly na baada ya hapo hatua zaidi za kuanza kufanya maandalizi ya ujenzi zitaanza kufanyika.

Ripoti ya bajeti ya ujenzi huo inaonekana kuwa tofauti na jinsi Trump alivyokuwa akizungumza wakati wa kampeni za kutafuta Rais wa nchi hiyo kwani alitarajia kuwa ujenzi huo utagharimu Dola Bilioni 12 pekee ili ajenge ukuta ambao anaamini utakuwa na faida kwa usalama wa Marekani.

Share:

Leave a reply