Trilioni 48 kutumika kutekeleza Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa

876
0
Share:

Kiasi cha Shlilingi Trilioni 48 kinahitajika kutoka Sekta Binafsi ili kufanikisha ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo kupitia Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa unaotekelezwa kuanzia mwaka wa fedha wa 2016/2017 hadi mwaka 2020/2021

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, amesema hayo mjini Dodoma wakati akifunga semina ya siku moja iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi hapa nchini-TPS iliyohusu zitaugharimiaji mkubwa wa miradi ya ubia kati ya sekta ya Umma na Sekta Binafsi kupitia mradi wa TVC (Tanzania Venture Capital and Private Equity Project)

“Imekadiriwa kuwa mahitaji ya fedha ya mpango huo ni takriban shilingi Trilioni 107, kati ya hizo shilingi Trilioni 59, sawa na asilimia 55, zitatokana na mapato ya Serikali na shiilingi Trilioni 48, sawa na asilimia 45 zitatokana na vyanzo vya Sekta Binafsi,” alisema Mpango.

Amesisitiza umuhimu wa Sekta Binafsi kuwekeza zaidi kwenye kilimo na viwanda vitakavyosaidia kuongeza thamani ya mazao ya wakulima ili waweze kunufaika kiuchumi  na kuendeleza nchi kwa ujumla.

Dkt. Mpango, ameahidi kuwa Serikali iko tayari kuhakikisha kuwa vitendea kazi muhimu vya utekelezaji wa mradi huo vinapatikana ili kuwezesha utekelezaji wa miradi hiyo ya ubia ukiwemo mradi wa ujenzi wa barabara ya njia sita kutoka Dar es salaam kwenda Chalinze.

Benny Mwaipaja, Dodoma

Share:

Leave a reply