Trump aitaka UN kuiwekea vikwazo vipya Korea Kaskazini

658
0
Share:

Rais wa Marekani, Donald Trump amelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuiwekea vikwazo vipya Korea Kaskazini.

Rais Trump amefikisha ombi lake hilo kwa UN wakati alipokutana na mabalozi 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika Ikulu ya White House mkutano uliohudhuriwa na wawakilishi wa China na Urusi.

“Baraza lazima liandae vikwazo vipya na vilivyo na nguvu kwa Korea Kaskazini kuhusu nyuklia na makombora wanayorusha,”  alisema Trump na kuongeza.

“Korea Kaskazini ni tatizo kubwa duniani na hatimaye tumelipatia jibu, wengi wamejitia upofu kwa muda mrefu lakini sasa ni muda wa kulimaliza.”

Share:

Leave a reply