Trump apendekeza pesa za USAID zipunguzwe

423
0
Share:

Rais wa Marekani, Donald Trump ametoa mapendekezo katika bajeti ya Marekani ya kupunguza pesa ambazo zinazotengwa kwa ajili ya vitengo vya Ikulu ya Marekani na Shirika la Misaada la Marekani (USAID).

Pendekezo la Trump linaelezwa kuwa ni kupunguza bajeti kwa asilimia 28 kutoka ilivyo sasa ya Dola Bilioni $36.7, na kupendekeza bajeti ya Dola Bilioni $25.6 kwa vitengo vya Ikulu ya Marekani na USAID.

Mapango mengine wa Trump ni kupunguza pesa ambazo imekuwa ikitoa kwa ajili ya bajeti ya Umoja wa Mataifa (UN), kwa sasa ni asilimia 22 ya bajeti ya Umoja wa Mataifa na 28.5 kwa ajili ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa.

Trump hajasema moja kwa moja mapendekezo yake katika hilo lakini ikielezwa kuwa kama itatoa pesa basi haitakuwa zaidi ya asilimia 25 kwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa ambao bajeti yao inatajwa kufikia Bilioni 7.9.

Share:

Leave a reply