Trump kutoa agizo jipya la kuzuia wahamiaji kuingia Marekani

628
0
Share:

Baada ya agizo la kwanza la kuzuia wahamiaji na wakimbizi kutoka katika mataifa saba yenye imani kali ya Kiislamu kutenguliwa na mahakama, Rais wa Marekani, Donald Trump amesema atatoa agizo lingine.

Trump amesema agizo hilo atalitoa wiki ijayo na litakuwa lenye nguvu ambalo anaamini mahakama ya nchi hiyo haitaweza kulitengua kama jinsi ambavyo walifanya katika agizo la kwanza.

“Agizo mpya litawagusa walengwa moja kwa moja kwa jambo ambalo nakusudia kuwa ni maamuzi mabaya,” alisema Trump na kumalizia kwa kusema “Tuna mahakama mbaya.”

Aidha pamoja na Trump kuweka wazi mpango wake wa kutoa agizo mpya lakini hajasema agizo hilo litagusa maeneo gani lakini akisisitiza agizo hilo ni kwa ajili ya usalama wa Marekani.

Share:

Leave a reply