Tukio la kupatwa kwa mwezi jioni ya leo Agosti 7,2017

1425
0
Share:

Kupatwa kwa mwezi ni tukio linaweza kutokea mara kadhaa kwa mwaka na halina athari yoyote kwa hali ya hewa.

Tukio hili hutokea pale Dunia, katika mizunguko yake, inapokuwa kati ya Jua na Mwezi; hali hii husababisha Dunia kuikinga miali ya Jua ielekeayo katika mwezi na hivyo kivuli cha Dunia kuonekana katika Mwezi. Ikiwa kivuli cha Dunia kitaonekana katika upande mmoja wa Mwezi basi hali hii huitwa kupatwa kiasi kwa Mwezi (yaani partial lunar eclipse). Kwa upande mwingine, ikiwa kivuli chote cha Dunia kitaonekana katika uso wa Mwezi basi hii huitwa kupatwa kamili kwa Mwezi (yaani total lunar eclipse).

Kwa ujumla kupatwa kwa Mwezi huwa hakuna athari kubwa katika hali ya hewa. Hata hivyo, kutokana na Mwezi, Dunia na Jua kukaa katika mstari mmoja, nguvu za uvutano huongezeka na hivyo kuweza kusababisha maji ya bahari kupwa na kujaa kwa kiasi kikubwa kuliko ilivyo kawaida.

Jioni ya leo tarehe 7 Agosti 2017, kati ya saa 2:22 hadi saa 4:18 usiku, Mwezi unatarajiwa kupatwa kiasi (yaani partial lunar eclipse) ambapo kilele chake kinatarajiwa kuwa saa 3:20. Hali hii inatarajiwa kuonekana kutoka katika maeneo mengi ya Dunia ikiwemo yote ya Tanzania.

Kama ilivyoainishwa hapo awali, kwa ujumla hali hii huwa haina athari kwa hali ya hewa ila tu uwezekano wa maji ya bahari kupwa na kujaa kwa kiasi kikubwa kuliko ilivyo kawaida.

Imetolewana

Mamlakaya Hali ya Hewa Tanzania

Share:

Leave a reply