Tundu Lissu aachiwa kwa dhamana ya milioni 10

596
0
Share:

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alhamisi ya Julai, 27 imemuachia kwa dhamana ya milioni kumi Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu.

Tundu Lissu amepewa dhamana yenye masharti ya kumtaka kutotoka nje ya Dar es Salaam huku kesi yake ikihairishwa hadi Agosti, 24 ya mwaka huu.

Mwanasheria huyo wa Chadema alikamatwa Julai, 20 akiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere alipokuwa akielekea nchini Rwanda kwenye mkutano wa Marais wa vyama vya mawakali wa Afrika Mashariki.

Share:

Leave a reply