Tuzo za Forbes kutolewa jioni ya leo Jijini Nairobi, Rais Magufuli akiwa juu kwa asilimia 84

356
0
Share:

Tayari watu maarufu, wakiwemo wafanyabiashara, viongozi wa Serikali na wadau wengine wapo Jijini Nairobi Nchini Kenya katika tukio maalum linalotarajia kufanyika jioni hii ya leo Novemba 17.2016 ya utoaji wa tuzo za heshima ya Forbes Afrika kwa mwaka 2016 (Forbes Africa’s Person Of The Year 2016).

Awali mpaka wanafunga zoezi la upigaji wa kura, Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameweza kuongoza kwa kupata asilimia nyingi za kura zote zilizopigwa katika zoezi hilo la awali ambapo aliweza kufikisha kura asilimia 84.

Rais Magufuli  aliingia katika kinyang’anyiro hicho cha kuwania tuzo hiyo kutokana na mapambano yake ya kuinua uchumi wa nchi tokea alipoingia madarakani ambapo ni kwa muda wa mwaka mmoja sasa.

Wengine na kura zao kwenye mabano ni i Mwanzilishi wa Benki ya Capitec ya Afrika Kusini, Michiel Le Roux ( 1%), Mwendesha Mashtaka wa Umma, Thuli Madonsela wa Afrika Kusini (2% ), Rais wa Mauritius, Ameenah Gurib anayepambana kulinda mazingira nchini mwake ( 1% ) na mwisho ni Wananchi wa Taifa la Rwanda kwa hatua iliyofikiwa na serikali ya nchi hiyo kwa ajili ya kupigania usawa wa kijinsia (12).

Kwa ujumla kura zilipigwa kupitia mtandao huo wa Forbes kupitia mtandao wa poy2016.com

Kwa mwaka jana tuzo hiyo ilinyakuliwa na Mtanzania, mfanyabiashara Mohammed Dewji  ‘MO’ ambaye ni  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL  Group). Kihistoria tuzo  hizo zilianza kutolewa mwaka 2011 na tangu kutolewa kwake zimekuwa zikiwavutia watu mashuhuri na waliofanya mengi katika kukuza uchumi wao na mataifa yao.

Endelea kufuatilia mtandao huu  tutakuletea kila kinachotokea katika tukio hilo jijini Nairobi

cxd0x3hwiaaxl7tKura zilizopigwa hadi  kufungwa kwa zoezi

cxos2lqxaaatybwWashiriki waliokuwa wameingia katika kinyang’anyiro hicho

Baadhi ya washindi waliowai kushinda tuzo hizo tokea zimeanzishwa 

Share:

Leave a reply