Tweet ya Rais Magufuli kumpongeza Uhuru Kenyatta

445
0
Share:

Baada ya Uhuru Kenyatta kutangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi mkuu wa Kenya 2017 na hivyo kupata tiketi ambayo itamwezesha kuiongoza Kenya kwa muhula wa pili tayari ameanza kupokea salamu za pongezi kutoka kwa nchi jirani za Kenya.

Rais wa kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki kumpongeza alikuwa ni Rais wa Rwanda, Paul Kagame akafuatia Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kisha Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Salamu zote za viongozi hizo zimetumwa kupitia Twitter ambapo kwa Rais Magufuli aliandika, “Nakupongeza Ndg.Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Kenya kwa kipindi kingine. Nakutakia mafanikio mema.”

Share:

Leave a reply