UAE yawabana raia wake wanaoionea huruma Qatar

446
0
Share:

Mwanasheria Mkuu wa Falme za Kiarabu (UAE), Hamad Saif Al-Shamsi ametangaza kuwa ni kosa la kisheria kwa raia yoyote wa nchi hiyo ambaye ataonyesha huruma dhidi ya Qatar kwenye mitandao ya kijamii.

Shamsi amewataarifu watumiaji wa mitandao ya kijamii kuwa kosa hilo litakuwa la matumizi mabaya ya mitandao na kwa atakayekutwa na hatia ya kufanya kosa hilo atahukumiwa kifungo cha miaka 15 au alipe faini ya Dirhams 500,000 ambazo ni sawa na Dola $136,000 sawa na Tsh. 304 milioni.

Mwanasheria Mkuu huyo amesema uamuzi huo umekuja baada ya Qatar kushutumiwa na baadhi ya mataifa ikiwepo UAE wenyewe kuwa inasaidia ugaidi.

Aidha katika hatua nyingine nchi ya Mauritania imekuwa nchi ya nane kukata uhusiano wake na Qatar baada ya nchi ya Saudi Arabia, Falme za Kiarabu (UAE), Bahrain, Misiri, Yemen, Maldives na Mauritus.

Pia jumanne ya Juni, 6, Rais wa Marekani, Donald Trump aliunga mkono hatua zinazochukuliwa dhidi ya Qatar na kuwa hizo ni hatua za kumaliza ugaidi duniani.

Share:

Leave a reply