Ubalozi wa China wakabidhi madawati 300 Iramba Magharibi

277
0
Share:

Ubalozi wa China nchini pamoja na shirikisho la wachimbaji wadogo wa madini Tanzania, umetoa msada wa madawati 400 yenye thamani ya shilingi 28 milioni kwa shule za msingi jimbo la Iramba Magharibi.

Ubalozi wa China umetoa msada wa madawati 300 yenye thamani ya shilingi 21 milioni, wakati shirikisho la wachimbaji madini wadogo Tanzania limetoa msaada wa madawati 100 yenye thamani ya shilingi saba milioni, Gharama ya madawati hayo , ni shilingi 70,000 kwa dawati moja.

Hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika juzi kwenye viwanja vya Ofisi ya halmashauri ya wilaya ya Iramba iliyopo New Kiomboi mjini hapa.

Akizungumza kwenye makabidhiano hayo, balozi wa China nchini, Dk Luq Youg’ng, alisema kwamba msaada huo wa madawati walioutoa wakishirikiana na shirikisho la wachimbaji wadogo, ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli, kuwa ifikapo Juni 30 mwaka huu, pasiwepo na mwanafunzi wa shule ya Msingi na sekondari, atakayekaa sakafuni au juu ya tofali wakati wa masomo. 

“Nimefurahishwa mno na juhudi za serikai ya awamu ya tano za kutoa kipaumbele kwenye sekta ya elimu. Hatua hii itaisadia mno Tanzania kuharakisha upatikanaji wa maendeleo endelevu’” alisema balozi huyo.

Akisisitiza,alisema kutokana na umuhimu wa sekta ya elimu kwa maendeleo ya nchi yoyote duniani, nchi ya China imejiwekea utamaduni wa kuwalipa mishahara ya walimu kwanza, kabla ya watumishi wengine.

“Sio hivyo tu, ujenzi wa majengo ya shule na vyuo vya elimu nayo yamepewa kipaumbele…. yaani yanajengwa kwanza na yakikamilika,ndipo ujenzi wa majengo ya idara zingine za serikali yaanze kujengwa. Kwa maamuzi hayo, utaona ni jinsi gani china inavyojali sekta ya Elimu,” alifafanua balozi huyo.

Na Nathaniel Limu, Iramba

IMG_5779

Mkuu wa wilaya ya Iramba, Lucy Mayenga, akitoa taarifa yake kwa balozi wa China nchini, Dk.Lug Youg’ng (wa kwanza kushoto) aliyetembelea wilaya hiyo juzi.Anayeangalia kamera ni mkuu wa mkoa wa Singida mhandisi Mathew Mtigumwa.

IMG_5782

Mkuu wa wilaya ya Iramba, Lucy Mayenga, akitoa taarifa yake kwa balozi wa China nchini, Dk.Lug Youg’ng (wa kwanza kushoto) aliyetembelea wilaya hiyo juzi.Anayeangalia kamera ni mkuu wa mkoa wa Singida mhandisi Mathew Mtigumwa.

IMG_5792

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi na mbuge wa jimbo la Iramba Magharibi, Mh. Mwigulu Nchemba, akitoa shukrani zake kwa wapiga kura wake kwa kumpigia kura za kutosha zilizomsaidia kutetea nafasi yake na kuteuliwa kuwa waziri.

IMG_5810

Balozi wa China nchini, Dk.Lug Youg’ng, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika juzi kwenye viwanja vya ofisi mkuu ya halmashauri ya wilaya Iramba. Pamoja na mambo mengine,alisema Watanzania wamelamba dume kwa kumchagua Dk.John Pombe Magufuli kuwa rais ambaye anatekeleza majukumu yake kwa kiwango cha juu mno.Pembeni ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi na mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi, Mh. Mwigulu Nchemba.

IMG_5812

Balozi wa China nchini, Dk.Lug Youg’ng, akikata utepe ikiwa ni sehemu ya makabidhiano ya msaada wa madawati 400 yenye thamani ya zaidi ya shilingi 28 milioni kwa shule za msingi wilaya ya Iramba. Ubalozi wa China umetoa msaada wa madawati 300 na mengine 100 yametolewa na shirikisho la wachimbaji wadogo wa madini Tanzania.Wa kwanza kushoto ni mwenyekiiti wa CCM mkoa wa Singida, Martha Mlata na wa kwanza kulia ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi na mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi, Mh. Mwigulu Nchemba.

IMG_5826

Baadhi ya wananchi wa tarafa ya Ndago waliohudhuria mkutano wa hadhara ulioitishwa kwa ajili ya mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi, Mh. Mwigulu Nchemba kutoa shukrani kwa kuchaguliwa kwa kishindo kwenye uchaguzi mkuu uliopita. (Picha zote na Nathaniel Limu)

Share:

Leave a reply