Ubalozi wa Marekani kushirikiana na ZIFF katika mpango wa mabadilishano ya kitamaduni

835
0
Share:

Ubalozi wa Marekani  kwa kushirikiana na Waandaaji wa Tamasha la Kimataifa la Filamu za Nchi za Jahazi (ZIFF), mapema leo Mei  17.2017, wameingia ubia rasmi na kusaini  hati ya makubaliano (MoU) juu  ya mabadilishano ya Kitamaduni ambapo itahusisha kumleta Muongozaji wa filamu wa Kimarekani Judd Ehrlich na mtaalam wa filamu Debra Zimmerman.

Tukio hilo la kusaini makubaliano hayo limefanyika katika Ubalozi  huo wa Marekani Jijini Dar es Salaam, ambapo Kaimu  Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Bi. Virginia Blaser pamoja na Mkurugenzi wa ZIFF, Bw. Fabrizio  Colombo  waliweza kubadilishana hati hizo huku wakielezea namna mabadiliko makubwa katika tamasha la ZIFF 2017, kwani litakuwa la kipekee hasa wataalamu hao wa filamu kutoka Marekani ambao wanatarajia kuleta ujuzi kwa wasanii na waendesha filamu wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

 Bi Virginia amebainisha kuwa, nchi yake inawaleta wataalam hao wa masuala ya filamu  ili kuonesha uwezo wao pamoja na kutoa elimu katika tasnia ya filamu.

“Kupitia ubia huu sisi na ZIFF, wataalam hao wa filamu watafanya  kazi moja kwa moja na watengenezaji wa filamu wa hapa Tanzania hasa visiwani Zanzibar ambao wanachipukia katika kipindi hicho cha tamasha hapo Mwezi Julai mwaka huu.” Alieleza Bi. Virginia.

Pia ameongeza kuwa, wamefurahia kuimarisha msaada wao hao kupitia watu wa Zanzibar kupitia program hiyo ya Mabadilishano ya kitamaduni   ambapo ameeleza kuwa, watatoa fursa watengenezaji wa filamu wa Kimarekani naa Kizanzibari  kutumia sanaa hii kama nyezo ya kushughulikia  masuala mbalimbali yaanayogusa jamii zao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa tamasha hilo, Fabrizio Colombo amepongeza ushirikianao huo na kuongeza kuwa,  ujio wa watalaam hao wa masuala ya filamu katika tamasha hilo ambalo kwa mwaka huu linatarajia kufanyika  Julai 8-16.2017, Visiwani Zanzibar, itawasaidia watayarishaji na waongoza filamu hasa wanaochipukia katika visiwa hivyo vya Zanzibar pamoja na Afrika Mashariki kwa ujumla kwani watapata uzoefu wa hali juu.

“Tunawashukuru Taifa la Marekani kwa ushirikiano huu. Tunaamini wataalam wataleta mabadiliko kupitia filamu hasa katika nyanja mbalimbali katika jamii.”amesema Fabrizio Colombo.

Tamasha la ZIFF mwaka huu 2017, ni la 20, tokea kuanzishwa kwake na ufanyika kila mwaka  katika viunga vya Ngome Kongwe, Unguja ambapo limekuwa likiwakutanisha watu mbalimbali kutoka pembe za Ulimwengu wakijumuika pamoja na kushuhudia filamu mbalimbali zikioneshwa sambamba na uwepo wa Makongamano, Warsha, biashara, mafunzo kwa Jamii, Pia uwepo majukwaa ya  Watoto, Wanawake (Panorama) pamoja na Muziki kutoka kwa vikundi na bendi mbalimbali za ndani na nje.

Kaimu  Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Bi. Virginia Blaser (kuhoto) akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) wakati wa kutiliana saini ya makubaliano hayo ya mabadilishano ya kitamaduni. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa ZIFF, Bw. Fabrizio  Colombo. Tukio lililofanyika Ubalozi wa Marekani Jijini Dar es Salaam, mapema leo Mei 17.2017.

Mkurugenzi wa ZIFF, Bw. Fabrizio  Colombo akizungumza katika tukio hilo la makubaliano juu ya mpango wa mabadilishano ya Kitamaduni kati ya Marekani na ZIFF. Kushoto kwake ni Kaimu  Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Bi. Virginia Blaser. Tukio lililofanyika Ubalozi wa Marekani Jijini Dar es Salaam, mapema leo Mei 17.2017.

Kaimu  Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Bi. Virginia Blaser (kuhoto) na Mkurugenzi wa ZIFF, Bw. Fabrizio  Colombo (kulia) wakisaini makubaliano hayo ya mabadilishano ya kitamaduni. Tukio lililofanyika Ubalozi wa Marekani Jijini Dar es Salaam, mapema leo Mei 17.2017.

Wakibadilishana hati hizo mara baada ya kusaini

(Picha zote na Andrew CHALE-MO BLOG).

Share:

Leave a reply