Uchafuzi wa mazingira watajwa kusababisha vifo vya watoto milioni 1.7

573
0
Share:

Shirika la Afya duniani (WHO) limesema shughuli mbalimbali ambazo zinasababisha uchafuzi wa mazingira zinasababisha vifo vya watoto wasio pungua milioni 1.7 walio na umri chini ya miaka mitano.

Taarifa ya WHO imeeleza kuwa uchafuzi wa mazingira umekuwa ukisababisha magonjwa mbalimbali kwa watoto ambayo yamekuwa yakisababisha vifo kwa watoto ikiwepo ugonjwa wa kuhara, malaria na homa ya mapafu kwa watoto (pneumonia).

Aidha viwanda vikubwa ambavyo vimekuwa vikisababisha uchafuzi wa mazingira kwa kutoa moshi mzito vimetajwa kuchangia kusababisha magonjwa ya moyo, mwili kupooza na kansa kwa watoto.

Mkuu wa Idara ya Afya ya Umma na Mazingira wa WHO, Maria Neira amesema shughuli za uchafuzi wa mazingira zimekuwa zikizidi kuongezeka na hivyo kuongeza athari kwa watoto hivyo ni vyema serikali ya kila nchi ikaangalia jinsi gani itapunguza shughuli hizo ili kuwalinda watoto.

Share:

Leave a reply