Udanganyifu wa idadi ya wakimbizi waiweka hatarini Uganda kupata misaada

100
0
Share:

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limetishia kusitisha msaada kwa serikali ya Uganda kwa madai kuwa, baadhi ya maofisa wake wanaongeza idadi ya wakimbizi tofauti na idadi halali iliyokuwepo kwa ajili ya kuiba fedha. 

UNHCR imesema wafadhili wake watazuia msaada wa fedha kwa operesheni za Uganda hadi idadi ya wakimbizi ithibitishwe baada ya uwepo wa tuhuma za maafisa hao kuongeza idadi halali ya wakimbizi.

Kufuatia madai hayo, serikali ya Uganda, Umoja wa Mataifa na wa Ulaya wanafanya uchunguzi kuhusu madai hayo pamoja na uuzwaji wa vyakula na vifaa vya msaada vya wakimbizi kwa watu wa kawaida.

Share:

Leave a reply