Ufilipino yatangaza hali ya hatari baada ya mauaji ya watu 14 katika shambulizi la bomu

253
0
Share:

Rais wa Filipino Rodrigo Duterte ametangaza hali ya hatari baada ya mauaji ya watu 14 yaliyotokea kwenye mlipuko wa bomu katika mji wa Davao nchini humo.

Abu Sayyaf anayejiita mwenye msimamo mkali amedai kuhusika na shambulio hilo. Licha Sayyaf kutangaza kuhusika, mamlaka za usalama nchini humo zimeahidi kuangalia watuhumiwa wengine zaidi.

Mlipuko huo ulitokea majira ya usiku karibu na maeneo ya soko, chuo kikuu na hoteli yenye hadhi ya nyota, na kuua watu 14.

Chuo hicho kinachofahamika kwa jina la Ateneo de Davao University na hoteli Marco Polo, inadaiwa kutumiwa na rais Duterte kwenye ziara zake nyingi na hoteli hiyo ilitumika kwa ajili ya mikutano wakati wa kampeni za Uchaguzi wake wa kitaifa.

Rais Duterte aliviambia vyombo vya habari nchini humo kuwa, amelazimika kutangaza hali ya vurugu kutokana na vitendo vya kihalifu vilivyotokea nchini humo.

Duterte leo amewaambia waandishi wa habari katika mji wa Davao kuwa ‘Ni tishio dhidi ya watu na dhidi ya taifa nitachukua hatua kali dhidi ya waliohusika na shambulio hilo, nina wajibu huu ili kulinda nchi hii .’

Msemaji wa Abu Sayyif alisema walihusika na mlipuko huo, na kudai kuwa Kundi linaloongozwa na Sayyif limetishia kuanzisha mashambulizi baada ya wapiganaji wake 30 kuuawa katika mashambulizi ya kijeshi yaliyotokea wiki iliyopita.

Hata hivyo, Duterte amesema wakaguzi wanaendelea kuangalia watuhumiwa wengine zaidi ili kuthibitisha kama wahalifu wa dawa za kulevya walihusika.

“Hizi ni nyakati za ajabu, na mimi nina mamlaka ya kuruhusu vikosi vya usalama wa nchi hii kufanya upekuzi, na tutakabiliana na mgogoro uliopo sasa,”

Aliongeza. “Kuna mgogoro katika nchi na washirika wa madawa ya kulevya, ambao wanafanya mauaji yasiyo halali na inaonekana kuwa bado kuna mazingira ya vurugu kutoka kwa wahalifu.”

Tangu uzinduzi wake kama rais wa kupambana na wafanyabiashara wa dawa za kulevya mwishoni mwa mwezi Juni,2016, watu 2,000 wameuawa hadi sasa.

Na Regina Mkonde

Share:

Leave a reply