Uingereza kupigwa faini na Umoja wa Ulaya (EU) ya Pauni Mil. 50

560
0
Share:

Nchi ya Uingereza inaweza kutozwa faini ya kiasi kisichopungua Pauni 50 billioni, (Dola za kimarekani 62.1 billioni) iwapo Waziri Mkuu wake, Theresa May atavunja kifungu cha 50 cha sheria za Umoja wa Ulaya na kuanza upya mashauriano ya mkataba mpya kati ya Umoja wa Ulaya na nchini yake.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa mashauriano wa Uingereza kujitoa Bw, Michel Barnier na baadhi ya maofisa wa Umoja Ulaya (EU) kupitia shirika la habari la Sky.

Shirika hilo la habari lilimnukuu, Barnier akisema kuwa Uingereza wanatakiwa kulipa Pauni 50 bilioni na inaweza kufika pauni 60 billioni ili kuanza mahusiano na mashirikiano mapya ya kiuchumi na kibiashara na umoja huo kutokana na hasara ya kujitoa kwa nchini hiyo kwenye umoja.

Mtoa taarifa mwingine aliliambia shirika hilo la habari la Sky kuwa, “tuliambiwa kiasi cha paundi 60 hadi 50 billioni kama faini baada ya kujitoa ndani ya umoja wa ulaya,”

Taarifa zinasema kwamba kiasi hicho cha pesa kinatokana na mchango mkubwa wa bajeti ya Uingereza ndani ya umoja huo na hii inasababishwa na hasara kwa kujitoa kwao katika maswala mazima ya bima, biashara za kifedha, riba, pensheni kwa wananchi wa umoja huo na malipo mengine ya mikopo ndani ya umoja huo.

Share:

Leave a reply