Ujumbe mzito wa wapiga picha kwa kampuni zinazotengeneza kamera

393
0
Share:

Waandishi wa habari za picha na watengenezaji wa filamu duniani wamejiunga kwa pamoja na kutuma ujumbe kwa ulimwengu juu ya umuhimu wa makampuni ya kutengeneza kamera kuboresha zana za kulinda vifaa katika matumizi ya kutafuta na kupiga picha kwa ajili ya vyombo vya habari.

Katika barua ya wazi iliyochapishwa na Taasisi ya Uhuru wa vyombo vya habari (Freedom of the Press Freedom), zaidi ya waandishi wa habari za picha 150 na watengenezaji wa filamu duniani waliwasihi kampuni za Nikon, Sony, Canon, Olympus na Fuji kuendeleza mifumo ya kutengeneza kamera zinazotoa picha bora kabisa.

Ingawa kila aina ya waandishi wa habari wanakabiliwa na hatari wakati wa kukusanya habari za matukio yenye utata au hatari, kazi ya wapiga picha na watengenezaji wa filamu ni ngumu katika mazingira ya wazi au kucheza filamu sehemu ya wazi au kuhifadhi data kwa ufanisi kwenye kamera.

Hata hivyo, Kamera nyingi zipo nyuma ya nyakati za sasa juu ya kuweza kuchukua picha kwa ufasaha kwa mbali katika maeneo hatarishi kwa mwandishi wa habari za picha na sehemu ya nakala ya barua hiyo inasema โ€œ picha unayochukua inaweza kufanyia kazi kitafiti na polisi au majeshi au walinzi wa mipakani katika sehemu za nchini tunapokuwa safarini na madhara yakawa ni makubwa,โ€ ilisema sehemu ya barua hiyo.

Matatizo halisi ya dunia

Ukandamizaji huu wa vyombo vya habari kupitia kamera ni tatizo kubwa katika tasnia ya habari duniani na sehemu ya barua hii ni kuwasilisha malalamiko yetu kwa kampuni za kutengeneza kamera kuja na aina mpya za kudhibiti upenyo wa utoaji wa picha zetu kwa watu ambao wanahitajika kumulika na vyombo vya habari duniani.

Hii si tu kutokea katika maeneo ya vita au chini ya serikali za kimabavu, ila pia sehemu zingine ambazo hakuna machafuko wala utawala dikteta wapiga picha wana wakati mgumu wa kujulikana na maadui zao wawepo sehemu za kazi.

Barua hiyo ya wazi kutoka kwenye Taasisi hiyo ya Uhuru wa vyombo vya habari imekuja siku kadhaa baada ya waandishi na wapiga picha wa habari kutoka katika nchini mbalimbali kama vile Uturuki, Syria, Iraq, Zimbabwe na Somalia kuwa sehemu ya wanaowindwa zaidi na wengi wao kujeruhiwa au kuuwawa kabisa.

Share:

Leave a reply