Ukatili wa kingono wampeleka jela miaka 175 daktari olimpiki Marekani

155
0
Share:

Aliyekuwa daktari wa Timu ya Olimpiki ya Marekani, Larry Nasser amehukumiwa kwenda jela miaka 175 baada ya kukutwa na hatia ya makosa ya ukatili wa kingono dhidi ya wanawake na wanamichezo nchini humo.

Kwenye kesi hiyo mashahidi wapatao 160 waliwasilisha ushahidi wao ambapo Nasser alikiri kufanya makosa 10. Hata hivyo alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 60 jela kutokana na kukutwa na hatia ya kumiliki picha ya ngono za watoto kinyume na sheria.

Jaji Rosemary Aquilina amesema adhabu hiyo itakua fundisho kwa watu wengine kutokana na alichofanya Nasser.

Share:

Leave a reply