UN yaikosoa serikali ya Congo DRC

549
0
Share:

Umoja wa Mataifa (UN) imeikosoa serikali ya Congo DRC kwa kuruhusu kuvuja kwa video inayoonyesha wafanyakazi wawili wa UN walivyouliwa.

Akizungumza kuhusu tuki hilo, Msemaji wa UN, Stephane Dujarric alisema kutolewa kwa video hiyo kunaweza kuathiri uchunguzi wa tukio hilo na kusababisha madhara kwa ndugu wa marehemu.

“Video ni kielelezo cha tukio hatufikiri kama ilitakiwa kutolewa na wala tunafikiri kama ilitakiwa kuonyeshwa kwa watu,” alisema Dujarric.

Taarifa hiyo ya UN imekuja kufuatia vyombo vya usalama vya nchi hiyo kuwaonyesha waandishi wa habari video ambayo inaonyesha wafanyakazi wawili wa Umoja wa Mataifa walivyouawa.

Share:

Leave a reply