UN yaomba mataifa kutoa msaada wa chakula kwa wananchi wa Somalia

662
0
Share:

Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN)  Antonio Guterres ametoa wito kwa mataifa kutoa  msaada wa chakula kwa raia wa Somalia ili kupunguza baa la njaa linaloikabili nchi hiyo. Alitoa wito huo Machi 7, 2017 katika zaiara yake ya dharula aliyoifanya nchini Somalia.

Guterres alitoa wito huo baada ya kushuhudia mateso makali wanayoyapata watu wenye utapiamlo na waathirika wa ugonjwa wa kipindupindu alipotembelea wodi ya Baidoa iliyoko mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu  ikiwa ni mara ya kwanza kutembelea mji huo tangu alipoteuliwa kuwa mkuu wa UN.

Amesema janga hilo linahitaji kuchukuliwa hatua kubwa kutokana kwamba watu zaidi ya milioni sita ambao ni sawa na nusu ya wakazi wa mji huo wanahitaji msaada hasa wa chakula.

“Kila mtu tuliyemuona alihadithia mateso anayopata  na hakuna namna ya kuelezea, watu wanakufa kwa njaa dunia lazima ichukue hatua kukomesha janga hili,”  alisema baada ya kuona waathirika wa kipindupindu katika wodi ya Baidoa.

Share:

Leave a reply