UN yasisitiza habari kuwezesha uwajibikaji

308
0
Share:

IMEELEZWA kwamba uhuru wa vyombo vya habari na upatikanaji wa habari bila kikwazo ni dawa ya kuwajibisha viongozi wa umma kutekeleza ahadi walizotoa wakati wa kutafuta kazi au kula kiapo cha utumishi.

Aidha uhuru huo unapokuwapo unasaidia wananchi kutambua wajibu wao na pia malengo yatakayowezesha kubadili maisha yao kuwa bora zaidi na yenye furaha na amani.

Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakati akizungumza na wadau wa habari mjini Mwanza katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani, ambapo kitaifa yalifanyika jijini Mwanza.

UN RC Tanzania, Alvaro Rodriguez

Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa Mataifa katika maadhimisho hayo.

Alisema uwepo wa habari unasaidia wananchi kujitambua na kutambua mambo muhimu yatakayoweza kuwafanya kuwa na uamuzi sahihi kuhusu viongozi wao na wao wenyewe.

Alisema pamoja na umuhimu wa vyombo vya habari na uhuru wake waandishi wa habari wamekuwa wakifanyakazi katika mazingira magumu na hatarishi kutokana na kuwapo kwa sheria zinazokandamiza upatikanaji wa habari na pia kuwapo kwa watu wasiotaka habari zao mbaya kuvuja.

Aidha zipo serikali zinaozotumia mabavu kunyamazisha taarifa mbalimbali zinazoonesha uonevu katika jamii.

Kiongozi huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kwamba anasikitishwa na kuendelea kubanwa kwa uhuru wa habari na vyombo vya habari na kutaka serikali zote, wanasiasa, wafanyabiashara na wananchi kulinda uhuru wa vyombo vya habari na wanahabari wenyewe kwa manufaa ya jamii.

“ Bila kuhakikisha haki hii ya msingi inapatikana, wananchi watakuwa hawako huru na wala hawatakuwa na uwezo wa kujiendeleza. Kwa kuwapo uhuru huo tunaweza kufanyakazi pamoja na kujenga dunia yenye heshima na fursa kwa wote” alisema Bw. Rodriguez wakati akimkariri Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon.

Rodriguez alisisitiza katika hotuba yake hiyo kwamba uhuru wa kupata habari  ni mtambuka kwa maana unagusa masuala mengi ikiwa ni ukweli wa habari zenyewe na heshima kwa ubinadamu.

Alisema ajenda ya Umoja wa Mataifa kuhakikisha kwamba habari zinasaidia dunia kukabiliana na umaskini na kuipa maendeleo endelevu.

Sherehe za siku ya vyombo vya habari duniani imefanyika wakati dunia ikiwa inaadhimisha miaka 250 ya kuanza kutumika kwa sheria ya haki ya habari kama inavyotumika nchini Sweden na Finland na miaka 25 ya tamko la Windhoek la uhuru wa vyombo vya habari.

Aidha maadhimisho hayo yanafanyika wakati ni mwaka wa kwanza wa utekelezaji wa maendeleo endelevu.

Unesco Dar es Salaam, Zulmira Rodrigues

Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodrigues akitoa salamu za Unesco katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani, ambapo kitaifa yalifanyika jijini Mwanza.

Naye  Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues amesema kwamba amefurahishwa na kuwapo kwa mmoja kati ya watanzania wawili, Ndimara Tegambwage waliokuwepo Windhoek, Namibia kushudia kutiwa saini kwa Azimio la Windhoek kuhusu uhuru wa vyombo vya habari.

Alisema pamoja na maazimio mengi inasikitisha kwamba mpaka leo inabidi bado jamii inatakiwa kukumbushwa kuhusu haki ya binadamu ya kupata habari.

Alisema pamoja na ukweli huo UNESCO inafanyakazi na  mashirika mbalimbali kuhakikisha usalama wa waandishi wa habari na pia kufanya kazi na serikali mbalimbali kuhakikisha kwamba kuna mazingira salama na bora ya kupashana habari na wanahabari.

Aidha alisema kwa sasa nchini Tanzania wanakamilisha azimio la usalama kwa waandishi wa habari litakalosimama katika nyanja sita. Nyanja hizo ni pamoja na kuimarisha ushirikiano na serikali na taasisi nyingine kuachana na sheria kandamizi, kuwezesha itifaki za kiutendaji zenye kuwezesha uhuru katika uchunguzi wa kadhia mbalimbali na usalama.

World Press Freedom Day 2016, Mwanza Tanzania

Aidha kuna nyanja ya kuwezesha waandishi kufanyakazi zao bila kuingiliwa na kutishwa na pia kuwezesha kuwapo kwa mfumo wa kuwezesha waandishi kuwa na nafasi ya kujilinda na kuimarisha maadili kwa waandishi wa habari.

Kuwa na mpango wa kuwezesha mfumo wa ukusanyaji takwimu juu ya sera na usalama waandishi wa habari na wafanyakazi katika vyombo vya habari.

Alisema kwamba mambo yote hayo yanahusiana na malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu kwa kuwa bila kuwa na uhakika wa habari suala la maendeleo ni tatizo.

Nape Nnauye, Mwanza

Waziri wa Habari, Michezo, Sanaa na Utamaduni, Nape Nnauye akitoa salamu za serikali kwenye maadhimisho hayo.

Naye Waziri wa Habari, Michezo, Sanaa na Utamaduni, Nape Nnauye,  amesema kwamba ili kuwezesha uhuru wa habari na vyombo vya habari serikali ipo tayari kukaa pamoja na wadau wa sekta husika, ili kuangalia sheria zilizopo na kuhakikisha kwamba haziingilii uhuru wa vyombo vya habari na upatikanaji wa habari.

Aidha ili kuhakikisha uhuru huo haufanyiwi fujo, serikali ipo tayari kukaa na wadau kupitia muswada wa huduma ya habari na sheria ya upatikanaji wake kabla ya kuupeleka Bungeni.

Alisema kufuatia sheria ya magazeti ya 1976 kuonekana ni miongoni mwa sheria kandamiza kwa uhuru wa habari, lazima wadau hao waweze kuunda ‘timu’ ambayo itaenda mjini Dodoma kuonana na waziri na waandishi wa Bunge.

Alisema sheria hiyo ni moja ya chanzo cha kusimamisha matangazo ya moja kwa moja Bungeni.

Mh. Nape Nnauye

“Nakubaliana na hiyo changamoto, lakini napenda kuwashauri muunde timu ya watu kadhaa ili mje Bungeni Dodoma kuonana nasi, warusha matangazo wa Bunge na kutembelea studio yenyewe, kisha tuzungumze,” alisema Nape.

Nape alisema serikali itakaa chini ili kuona sheria zinazokwaza vyombo vya habari zinafanyiwa kazi: Kauli mbiu ya mwaka huu ya maadhimisho hayo ni, kupata taarifa ni haki yako ya msingi, idai.

Alisema lazima yakusanywe maoni na kufikishwa Bungeni ili yaweze kufanyiwa kazi mawazo ya wadau wote ili kutopuuzwa na wazo lolote, lengo ni kutaka kuona uhuru wa vyombo vya habari unafanikiwa.

“Tukosoe bila uoga ili tuweze kusonga mbele kwani serikali na wadau wa habari si maadui,” alisema.

Dr. Reginald Mengi, MOAT

Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT), Dk. Reginald Mengi akitoa salamu za MOAT katika maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ambapo kitaifa yalifanyika jijini Mwanza.

Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT), Dk. Reginald Mengi, alisema ili vyombo vya habari viweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu, lazima serikali itoe uhuru wa kupata habari.

Dk. Mengi alisema vyombo vya habari haviwezi kutimiza wajibu wao kwa weledi kama watumishi wa umma watakataa au kughairi kutoa habari kwa visingizio vyovyote, hasa kwa madai ni siri ambazo hazipaswi kuchapishwa kwa usalama wa taifa.

Aidha, Dk. Mengi aliwataka waandishi wa habari kuandika habari za kimaendeleo na kuchochea uchumi wa nchi pamoja na kufahamu changamoto husika na jinsi ambavyo zinaweza kutatuliwa.

Alisema vyombo vya habari si adui wa jamii bali ni kioo cha jamii, hivyo lengo kubwa ni kuandika habari za ukweli na zile za furaha kwa jamii kuliko kuandaa za huzuni kila siku.

Pia, Dk. Mengi alisema vyombo vya habari vinatakiwa kujikita zaidi kuandika habari za mauaji ya albino na ujangili, lakini alishauri kufuatilia kwa undani watu wanaowatuma wauaji wa watu hao na tembo ili sharia iweze kuwabana.

Simon Berege, Misa-TAN

Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (Misa TAN), Simon Berege, akitoa salamu za Misa-TAN katika sherehe za maadhimisho ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani, ambapo kitaifa zilifanyika jijini Mwanza.

Awali Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (Misa TAN), Simon Berege, aliiomba serikali kufuta uamuzi wake wa kuzuia urushwaji wa matangazo ya Bunge ya moja kwa moja kutokana na kutokuwa na tija kwa Taifa.

Alisema sharia hizo ni namna nyingine ya kuminya haki ya wananchi kupata taarifa sahihi na kwa wakati kutoka kwa wawakilishi wao.

Robert Makaramba

Mgeni rasmi Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Mwanza, Robert Makaramba akisoma hotuba kwa niaba ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Chande Othman wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani, ambapo kitaifa yalifanyika jijini Mwanza.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Chande Othman, katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Mwanza, Robert Makaramba, alisema uwapo wa sheria nzuri za vyombo vya habari na upatikanaji wa taarifa ni chachu kubwa ya maendeleo nchini.

Jaji Makaramba alisema sheria hizo haziwezi kupatikana bila ya ushirikishwaji wa kina wa wadau husika na kutoa angalizo kwa serikali kuacha kung’ang’ania sheria zisizo rafiki kwa vyombo vya habari ili kuinua uhuru wa vyombo vya habari kidunia.

Hadi kufikia mwishoni mwa Aprili mwaka huu, Tanzania ilikuwa inashika nafasi ya 71 ya viwango vya uhuru wa vyombo vya habari kati ya nchi 180 duniani ambazo zimefanyiwa utafiti na taasisi ya wanahabari wasio na mipaka.

Maria Van Berlekom

Mkuu wa masuala ya Ushirikiano na Maendeleo kutoka Ubalozi wa Sweden Tanzania, Bi. Maria Van Berlekom akitoa salamu kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ambapo kitaifa yamefanyika jijini Mwanza.

Luana Reale, EU Tanzania

Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania, Luana Reale akitoa salamu za Umoja wa Ulaya kwenye sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani, ambapo kitaifa yalifanyika jijini Mwanza.

Jaji Robert Makaramba

Mratibu kutoka GEMSAT, Bi. Gladness Hemedi Munuo akimkabidhi mgeni rasmi Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Mwanza, Robert Makaramba kuzindua rasmi Sera ya Habari na Jinsia kwa vyombo vya Habari vya Jamii Tanzania katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani, ambapo kitaifa yalifanyika jijini Mwanza.

Uzinduzi

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Mwanza, Robert Makaramba akizindua rasmi Sera ya Habari na Jinsia kwa vyombo vya Habari vya Jamii Tanzania huku Waziri wa Habari, Michezo, Sanaa na Utamaduni, Nape Nnauye (kulia) na Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (Misa TAN), Simon Berege na viongozi wengine meza kuu wakishuhudia tukio hilo.

IMG_3518

Sera ya Habari na Jinsia kwa vyombo vya Habari vya Jamii Tanzania imezinduliwa rasmi.

Sera ya Habari na Jinsia kwa vyombo vya Habari vya Jamii Tanzania

Meza kuu ikionyesha Sera ya Habari na Jinsia kwa vyombo vya Habari vya Jamii Tanzania iliyozinduliwa rasmi katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani, ambapo kitaifa yalifanyika jijini Mwanza.

WPFD Tanzania 2016

Pichani juu na chini ni sehemu ya wahariri wa vyombo mbalimbali nchini, wanahari, wadau kutoka mashirika ya kimataifa waliohudhuria sherehe hizo jijini Mwanza.

Bakari Machumu

Abubakar Karsan

Onesmo Olengurumwa at the centre

Gladness Hemedi Munuo


Nape Nnauye

Waziri wa Habari, Michezo, Sanaa na Utamaduni, Nape Nnauye, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodrigues, Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT), Dk. Reginald Mengi, mgeni rasmi Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Mwanza, Robert Makarambaka wakiangalia burudani ya ngoma za asili iliyoambatana na mchezo wa nyoka aina ya Chatu.

Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi

Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT), Dk. Reginald Mengi akicheza na Chatu wakati wa burudani ya ngoma za asili katika wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani, ambapo kitaifa zilifanyika jijini Mwanza.

Simon Berege

Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT), Dk. Reginald Mengi na Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (Misa TAN), Simon Berege wakifurahi jambo wakati wa burudani ya ngoma za asili katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani zinazofanyika tarehe kila mwaka Mei 3, duniani kote, ambapo kitaifa zilifanyika jijini Mwanza.

Zulmira Rodrigues

Waziri wa Habari, Michezo, Sanaa na Utamaduni, Nape Nnauye, akiteta jambo na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia). Katikati ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT), Dk. Reginald Mengi wakijiandaa kwa zoezi la picha ya pamoja.

World Press Freedom Day Tanzania 2016, Mwanza

Mgeni rasmi Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Mwanza, Robert Makarambaka (katikati) katika picha ya pamoja na wadau wa tasnia ya habari  huku wakiwa wameshikiliza mabango ya malengo endelevu (SDG’s) wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani, ambapo kitaifa zilifanyika jijini Mwanza.

Dk. Reginald Mengi

Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT), Dk. Reginald Mengi akisamiana na waandishi wa habari wakongwe ‘Ma-veterans’ katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani, ambapo kitaifa zilifanyika jijini Mwanza.Katikati ni aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Kassim Mpenda.

Francis Nanai

Kutoka kushoto ni Mmoja wa waanzilishi wa mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo, Mhariri Mtendaji Mkuu wa Mwananchi Communications Limited, Bakari Machumu, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited, Francis Nanai katika picha ya ukumbusho kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani, ambapo kitaifa yalifanyika jijini Mwanza.

Colin Spurway

Mmoja wa waanzilishi wa mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo (kushoto) na Mkurugenzi Mkazi wa BBC Media Action nchini, Colin Spurway wakisapoti lengo #5 ‘Usawa wa Kijinsia’ la maendeleo endelevu (SDG’s) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani, ambapo kitaifa yalifanyika jijini Mwanza.

Dk. Mengi IPP Media

Baadhi ya wadau wa tasnia ya habari katika picha ya kumbukumbu na Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT), Dk. Reginald Mengi.

Alvaro Rodriguez SDG's

Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT), Dk. Reginald Mengi kwenye bango maalum la #WPFD2016 lililonakshiwa na rangi tofauti zinazowakilisha malengo ya maendeleo endelevu (SGD’s) kwenye sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani, ambapo kitaifa yalifanyika jijini Mwanza.

Head of Unesco Dar es Salaam and Representative, Zulmira Rodrigues

Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodrigues wakisapoti lengo #5 “Usawa wa Kijinsia”

Usia Nkhoma Ledama

Maafisa mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Usia Nkhoma Ledama na Hoyce Temu katika picha ya kumbukumbu na bango maalum la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani, ambapo kitaifa yalifanyika jijini Mwanza.

Neville Meena

Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Neville Meena katika picha ya pamoja na Wanamawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania.

Jane Mihanji

Afisa habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama na Makamu wa Rais wa UTPC, Jane Mihanji katika picha ya pamoja.

Share:

Leave a reply