Uongozi na wafanyakazi gazeti la Mwananchi wapaza sauti ya #BRINGBACKAZORY

409
0
Share:

Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania leo Desemba 7,2017 imetoa tamko la kuitaka Serikali na mamlaka zake kusaidia kupatikana kwa mwandishi wao wa kujitegemea wa gazeti hilo aliyekuwa akiripotia kutokea Kibiti Mkoani Pwani, ambapo amepotia kwa kuchukuliwa na watu wasiojulikana kwa muda wa siku 17, hadi leo hii.

Mkurugenzi wa gazeti la Mwananchi Francis Nanai akielezea mbele ya vyombo vya habari pamoja na uongozi na wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa pamoja ambao walivalia mavazi meusi na mabango ya ‘BringBackAzory, waliungana kwa pamoja katika tukio hilo.

Nanai ameviomba  vyombo vya ulinzi na usalama kuongeza juhudi za kumsaka Azory  kwa kutoweka kwake  kwa kipindi hicho cha zaidi ya siku 10.

“MCL ilipata taarifa za kupotea kwa Azory  tokea  Novemba 30,mwaka huu kutoka kwa ndugu zake na Mkewe. Tumefuatilia tukio hilo kwa vyombo vyote vya Ulinzi na mpaka leo hatujapata taarifa. Juhudi za kufuatilia zinaendelea kwa kutoa habari kwa vyombo vya ndani na nje. Pia tunaendelea kufanya hivyo huku pia tukiendelea kumfariji mkewe.

Pamoja na hayo, MCL imeandika barua kwa Waziri wa Habari, Spika wa bunge,TEF, MCT, Vituo vya sheria na haki za Binadamu na wadau wengine kuhusu kupotea kwa mwandishi wetu” alieleza Nanai.

Imeelezwa kuwa, Azory alianza kulitumikia gazeti hilo kama mwandishi wa kujitegemea kuanzia 2015 mpaka sasa kutoweka kwake.

Nanai  amebainisha kuwa, kwa kuwa hawajui ameshikiriwa na nani ama kwa kosa gani, wanaomba kumpata mwenzao akiwa hai ama mzima na mwenye afya njema ili waungane nae katika majukumu yake ya kila siku.” Alieleza Nanai katika taarifa yake hiyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti ya jukwaa la wahariri Teofile Makunga ambaye aliungana na MCL, aliomba mwandishi huyo kama anashikiliwa na watu basi aachiwe ama apelekwe mahakamani.

“Kama mwenzetu ameshikiliwa na vyombo vya usalama kwa sababu yoyote angetakiwa kuwa amefikishwa mahakamani kufikia sasa. Lakini kwa kimya hiki cha siku 17, zinatia mashaka na kutishia tasnia ya habari hapa nchini”alieleza Makunga.

Hata hivyo, tayari wadau wa habari wanatarajia kufanya maandamano ya kushinikiza kuzidishwa kazi kwa msako huo yatakayoanzia mnazi mmoja hadi makao makuu ya wizara ya mambo ya ndani jijini Dar es Salaam kwa nia ya kufikisha ujumbe kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro.

Na Andrew Chale,MO BLOG

Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya MCL, wakiwa katika nyuso za huzuni wakati wa tukio hilo

Mkurugenzi wa gazeti la Mwananchi Francis Nanai akisoma taarifa maalum juu ya tukio hilo mbele ya vyombo vya habari pamoja na uongozi na wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa pamoja mapema leo Desemba 7,2017, katika makao makuu ya kampuni hiyo Tabata Relini Jijini Dar es Salaam

Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya MCL, wakiwa katika tukio hilo

Mwenyekiti ya jukwaa la wahariri Teofile Makunga ambaye aliungana na MCL, katika tukio hilo akitoa tamko.

Mwandishi Mwandamizi wa Mtandao wa habari za mtandaoni wa MODEWJI BLOG, Andrew Chale akiwa ameungana na Mwandishi wa MCL, Salome Gregory katika kupaza sauti ya kuongeza juhudi ili apatikane mwandishi wa Mwananchi aliyepotea kwa siku 17 sasa Ndugu Azory Gwanda wa Kibiti, Mkoani Pwani

Wanahabari wakifuatilia tukio hilo

Mwenyekiti ya jukwaa la wahariri Teofile Makunga ambaye aliungana na MCL, katika tukio hilo akitoa tamko.

Mkurugenzi wa gazeti la Mwananchi Francis Nanai akisoma taarifa maalum juu ya tukio hilo mbele ya vyombo vya habari pamoja na uongozi na wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa pamoja mapema leo Desemba 7,2017, katika makao makuu ya kampuni hiyo Tabata Relini Jijini Dar es Salaam( PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE,MO BLOG)

Share:

Leave a reply