Uongozi wa Simba SC wapanga kufanya mazungumzo na MO Dewji

1878
0
Share:

Uongozi wa Simba SC umetoa taarifa kuhusu mwenendo ya klabu hiyo kwa sasa kufuatia kutokea mgawanyiko kwa mashabiki na wanachama wa klabu hiyo wengine wakisapoti uongozi wa klabu hiyo kuingia mkataba na kampuni ya ubashiri ya SportPesa na wengine wakilaumu uongozi kwa kuvunja makubaliano na mwanachama wa timu hiyo ambaye amepanga kufanya uwekezaji, Mohammed Dewji ‘MO’.

Taarifa ya Simba SC imetolewa kupitia ukurasa wa Instagram wa klabu hiyo na kuelezea kuwa tayari viongozi wamekutana kulizungumzia jambo hilo na hivi karibuni wamepanga kukutana na MO Dewji ili kuzungumzia mapungufu yaliyojitokeza na kuweka mpango mkakati ili kuhakikisha mpango wa mfanyabiashara huyo kufanya uwekezaji kwenye klabu hiyo kongwe nchini unafanikiwa. Zaidi waweza kusoma taarifa ya Simba hapa chini.

“Simba ni shwari.
Uongozi jana usiku ulikaa kikao cha pamoja kujadili suala la Sportpesa na MO kama ambavyo sisi sote tumekuwa tukisoma katika mitandao mbalimbali.
Hanspoppe amerudi kwenye nafasi yake ya ujumbe wa kamati ya utendaji.
Hakuna kiongozi mwingine atakayejiuzulu nafasi yake.
Uongozi utakutana na MO muda wowote kuanzia sasa kwa kikao cha pamoja kujadili mapungufu yote yaliyojitokeza na kutengezeza njia sahihi ya kufanikisha malengo tuliyojiwekea

Kwa pamoja Uongozi kwa kushirikiana na wadau wote wa Simba SC waendelee na kampeni ya kushinda mechi mbili zilizo mbele yetu ikiwa pamoja na fainali ya FA Dodoma.

Kwa muda huu ni matumaini yetu kuwa kwa pamoja tutaelekeza dua na nguvu zetu katika mechi 2 zilizobakia.
Simba Nguvu Moja.”

Simba ni shwari. Uongozi jana usiku ulikaa kikao cha pamoja kujadili suala la Sportpesa na MO kama ambavyo sisi sote tumekuwa tukisoma katika mitandao mbalimbali. Hanspoppe amerudi kwenye nafasi yake ya ujumbe wa kamati ya utendaji. Hakuna kiongozi mwingine atakayejiuzulu nafasi yake. Uongozi utakutana na MO muda wowote kuanzia sasa kwa kikao cha pamoja kujadili mapungufu yote yaliyojitokeza na kutengezeza njia sahihi ya kufanikisha malengo tuliyojiwekea Kwa pamoja Uongozi kwa kushirikiana na wadau wote wa Simba SC waendelee na kampeni ya kushinda mechi mbili zilizo mbele yetu ikiwa pamoja na fainali ya FA Dodoma. Kwa muda huu ni matumaini yetu kuwa kwa pamoja tutaelekeza dua na nguvu zetu katika mechi 2 zilizobakia. Simba Nguvu Moja.

A post shared by Simba SC Tanzania (@simbasctanzania) on

Share:

Leave a reply