Urusi yafungiwa kushiriki Olimpiki 2018

308
0
Share:

Kamati ya kimataifa ya Olimpiki, imeifungia nchi ya Urusi kushiriki michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi itayofanyika katika jiji la Pyeongchang nchini Korea kusini mwakani.

Rais wa IOC Thomas Bach na bodi yake walitangaza adhabu hiyo jana jioni baada ya kukutana katika mji wa Lausanne nchini Switzerland, ambapo maamuzi hayo yamefikiwa baada ya uchunguzi wa miezi kumi na saba kukamilika.

Uchunguzi huo ulio ongozwa na Rais wa zamani wa IOC Samuel Schmid, umebaini kwamba Serikali ya Urusi ilihusika katika udanganyifu wa kuanda michuano ya olimpiki iliyofanyika nchini humo mwaka 2014 pamoja na udanganyifu kuhusu matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni.

Licha adhabu hiyo, wanariadha wa Urusi wanaweza shiriki michuano ya majira ya baridi kama wanariadha huru ambao watakuwa wakiwakilisha nchi.

Share:

Leave a reply