Uvuvi wa kisasa waongeza kipato kwa wavuviKigoma

365
0
Share:

Baada ya Wavuvi wanaofanya shughuli zao katika ziwa Tanganyika mkoani Kigoma kuanza kutumia teknolojia katika shughuli ya uvuvi kutoka matumizi ya kalabai ya mafuta mpaka kutumia taa za sola, imewafanya wavuvi kunufaika katika shughuli yao ya uvuvi sambamba na kumaliza tatizo la uchafuzi wa mazingira uliokuwa ukisababishwa na moshi wa kalabai.

Kauli hiyo imetolewa na afisa uvuvi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Azizi Daud ambaye amesema kuwa  teknolojia hiyo ni rafiki kwa  mazingira na  imepelekea kuepuka gharama kubwa za kununua mafuta ya taa na badala yake kuchagi betri za sola kwa gharama kidogo.

Aidha Daudi amesema uvuvi huo umechangia kuongeza asilimia kubwa ya mapato ya uvuvi katika ziwa Tanganyika kwa utafiti uliofanyika mwaka 2011 japo kuwa kuna aina nyingine za uvuvi.

“Uvuvi wa kitaalamu uko wa aina nyingi na moja wapo ni hii inayotumika katika Ziwa Tanganyika na tayari tumeshaanza kuona faida kwa wavuvi kujipatia kipato sambamba na serikali kujiingizia mapato,” amesema Daud.

Hata hivyo Daud amewataka wavuvi kuendelea kuzingatia sheria za uvuvi na kuhakikisha hakuna mvuvi ambaye bado anatumia kalabai ya mafuti wakati wa uvuvi.

Na Emmanuel Senny, Kigoma

Share:

Leave a reply