Uwasilishwaji wa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (Picha)

287
0
Share:

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye leo amewasilisha bungeni bajeti ya wizara yake.

Mo Blog imekuandalia habari picha wakati wa uasilishwaji wa bajeti hiyo.

PICHA 1

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Nape Nnauye (Mb) (kulia) akiwa pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki wakiingia ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya usomwaji wa Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

PICHA 3

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (Mb) (kulia) akiwa pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki wakiwasili katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya usomwaji wa Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

PICHA 5

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Nuru Mrisho (kushoto) pamoja na Kaimu Mkurugenzi, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Zamaradi Kawawa wakiwa katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kwa ajli ya kusikiliza Bajeti ya Wizara hiyo leo.

PICHA 14

Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole-Gabriel (kulia), Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Nuru Mrisho (katikati) pamoja na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN), Zulmira Rodriguez wakifuatilia uwasilishwaji wa Bajeti ya Wizara hiyo 13 Mei, 2016 Bungeni mjini Dodoma.

PICHA 18

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Nape Nnauye akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake Bungeni mjini Dodoma.

PICHA 20

Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,Profesa Elisante Ole-Gabriel (katikati), Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara hiyo, Bi. Zawadi Msalla (kushoto) pamoja na Katibu wa Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Bi, Anna Nkinda wakifuatilia uwasilishwaji wa Bajeti ya Wizara hiyo.

PICHA 23

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Nape Nnauye (kushoto) pamoja na Naibu Waziri wake, Mhe. Anastazia Wambura wakijadiliana mara baada ya kuwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo Bungeni mjini Dodoma.

PICHA PAMOJA 1

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Nape Nnauye (mwenye tai nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja na Kundi la Wasanii na Bloggers Bungeni mjini Dodoma 13 Mei, 2016.

Share:

Leave a reply