Valencia yamfungashia virago kocha wake, Gary Neville

197
0
Share:

Klabu ya Valencia ya Hispania, imetoa taarifa jioni ya leo kuwa wamemtimu kazi aliyekuwa kocha wao, Gary Neville kufuatia kupata matokeo yasiowaridhisha.

Neville ambaye amedumu kwa miezi mitatu na siku kadhaa katika klabu hiyo tangu Disemba 2 mwaka jana, nafasi yake itachukuliwa na kocha wa zamani wa klabu hiyo, Pako Ayestaran ambaye ataiongoza hadi mwisho wa msimu.

Katika michezo 16 ambayo Neville ameiongoza Valencia amepata ushindi michezo mitatu pekee, sare michezo mitano na kupoteza michezo nane. Kwa sasa timu hiyo ipo nafasi ya 14 na ipo juu kwa alama sita kutoka kwa timu iliyo mkiani.

Share:

Leave a reply