VIDEO: Hispania yazindua makumbusho ya chini ya maji

1090
0
Share:

Katika hali ambayo inaonekana kuwavutia watu wengi, Hispania imefungua makumbusho ambayo yapo chini ya maji ambapo kama mtu akitaka kuyaangalia inambidi aingie ndani ya maji ili kuona makumbusho hayo.

Makumbusho hayo yapo katika Kisiwa cha Lanzarote kinachopatikana katika bahari ya Atlantic na yamepewa jina la Makumbusho ya Atlantic ambapo ndani yake kuna sanamu zaidi ya 300.

Makumbusho ya Atlantic yalianza kutumia tangu mwezi Machi, 2016 lakini yalikuwa bado hayajakamilika na sasa yamekamilika kwa kila kitu na kama mtu anakuwa anataka kwenda kuona makumbusho hayo anatakiwa kulipa Dola 49.

Share:

Leave a reply