VIDEO: Hotuba ya Rais Magufuli katika hafla ya kumwapisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi

3139
0
Share:

Jumatatu ya Februari 6, 2017 imeingia katika historia ya Tanzania kwa kuapishwa kwa Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Luteni Jenerali Venance S. Mabeyo ambaye ameapishwa na Rais John Magufuli akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Davis Mwamunyange ambaye amestaafu.

Baada ya zoezi la kumwapisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Rais Magufuli alitoa hotuba ambayo ilizungumzia namna alivyomteua mkuu wa majeshi ya ulinzi na namna taifa linavyopoteza nguvu kazi ya vijana kutokana na kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya na kuwataka Watanzania wote kuungana kupinga biashara hiyo kwani ina athari kwa jamii nzima ya Tanzania.

Zaidi waweza kutizama hotuba ya Rais Magufuli hapa chini.

Share:

Leave a reply