VIDEO: Magoli ya mchezo wa kwanza EPL 17/18 Arsenal Vs Leicester City

1127
0
Share:

Pazia la Ligi Kuu ya Uingereza 2017/2018 tayari limefunguliwa kwa washika bunduki wa London, Arsenal wakiwakaribisha Leicester City katika dimba la Emirates, mchezo uliomalizika kwa Arsenal kuibuka na ushindi wa goli 4-3.

Mshambuliaji mpya wa Arsenal, Alexandre Lacazette amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga goli katika msimu mpya wa Ligi kwa kufunga goli dakika ya 2 na magoli mengine ya Arsenal yakifungwa na Danny Welbeck dakika ya 45, Aaron Ramsey dakika ya 83 na Olivier Giroud katika dakika ya 45.

Kwa upande wa Leicester City magoli yake yalifungwa na Shinji Okazaki dakika ya 5 na mengine mawili yakifungwa na Jamie Vardy katika dakika ya 29 na dakika ya 56, waweza kuangalia magoli yote saba yaliyofungwa katika mchezo huo hapa chini.

Share:

Leave a reply