VIDEO: Makonda amwomba Rais Magufuli kutenga eneo la kuzika viongozi wa kitaifa

339
0
Share:

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemuomba Rais John Magufuli kutenga eneo katika makao makuu ya nchi yaliyopo mjini Dodoma, kwa ajili ya kuhifadhi miili ya viongozi waliotoa mchango wao katika kuliletea Taifa maeneleo .

Makonda ametoa wito huo leo wakati akitoa salamu za rambirambi kwa familia ya Marehemu Samuel Sitta aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Novemba 7, 2016 nchini Ujerumani.

Amesema kuwa, ili kuhifadhi kumbukumbu za viongozi waandamizi wa nchi kwa vizazi vijavyo, ni vyema wanapofariki miili yao kuhifadhiwa sehemu moja ambayo itakua kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.

Marehemu Sitta aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amelitumikia taifa kama kiongozi katika nyadhifa mbalimbali serikalini kwa zaidi ya miaka 40.

Share:

Leave a reply