VIDEO: Michelle Obama ampigia kampeni Hilarry Clinton kwa Wamarekani

265
0
Share:

Mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama ametoa hotuba katika mkutano wa kwanza wa Chama cha Democratic kwa kumnadi mgombea urais kwa tiketi ya Democratic, Hillary Clinton na kuwatahadharisha Wamarekani kuhusu Donald Trump.

Akizungumza katika mkutano, Michalle Obama alisema kwa kipindi kirefu Marekani imekuwa nchi ambayo inamshikamano lakini kwa kipindi cha karibuni kumekuwepo na watu ambaye anataka kuwagawanyisha raia wa nchi hiyo.

Alisema kuwa Marekani inahitaji mtu ambaye atasimamia misingi ya nchi hiyo iliyoachwa na waasisi wa taifa hilo na anayeweza kudumisha ushirikiano uliopo baina ya wamarekani na mtu huyo si mwingine bali ni Hillary Clinton.

“Nataka rais ambaye atawafundisha watoto wetu kwamba kila mtu katika nchi hii ana nafasi yake. Rais ambaye kweli anaamini katika maono ambayo yaliwekwa na waasisi kwa miaka iliyopita, kwamba sisi wote tuliumbwa sawa . Kila mtu anahusika katika historia kubwa ya Marekani na hata wakati migogoro, hatupaswi kuwa katika tofauti baina yetu. tunasikilizana, tunasaidiana sababu tupo imara kwa pamoja,

“Kila asubuhi nikiamka katika nyumba zilizojengwa na watumwa, na kuwaangalia binti zangu, warembo wawili weusi na walio na akili, wakicheza na mbwa wao katika bustani ya White House, ” alisema na kuongeza “Na kwa sababu ya Hillary Clinton, binti zangu, na watoto wetu wote wa kike na kiume wanaweza kukubali kuwa mwanamke anaweza kuja kuwa rais wa Marekani,” alisema Obama.

Share:

Leave a reply