VIDEO: Moto wazuka katika jengo la Trump Tower, watu wawili wajeruhiwa

393
0
Share:

Watu wawili wamejeruhiwa baada ya moto kuzuka katika jengo la Trump Tower lililopo eneo la Manhattan mjini New York, Marekani.

Kikosi cha kuzima moto New York kimesema moto huo umesababishwa na hitilafu ya umeme.

Kupitia mtandao wa Twitter, mtoto wa Rais Donald Trump, Eric ametoa pongezi kwa kikosi cha kuzima moto kwa kuchukua hatua za haraka.

Jengo hilo linatumika kwa shughuli za biashara na makazi.

Share:

Leave a reply