VIDEO: Samsung yazindua simu ya Galaxy 8 na Galaxy S8+

1107
0
Share:

Kampuni ya vifaa vya kieletroniki ya Samsung imefanya uzinduzi wa simu mpya za Galaxy S8 na Galaxy S8 Plus ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kutoa bidhaa za Galaxy baada ya mwaka uliopita kutoa Galaxy S7 na Galaxy S7 Plus.

Simu za Galaxy S8 ina ukubwa wa inchi 5.8 na Galaxy S8 Plus ni inchi 6.2 huku zikiwa zimewekewa baadhi ya programu ambazo hazikuwepo katika Galaxy S7 na Galaxy S7 Plus.

Baadhi ya programu ambazo ni mpya ni programu saidizi ya kuzungumza ikifananishwa na programu ya Siri katika vifaa vya kampuni ya Apple na programu ya kuunganisha simu kutumia katika kompyuta.

Simu hizo zinatajwa kuwa zitauzwa Euro 689 kwa Galaxy S8 na kwa Galaxy S8 Plus itauzwa Euro 779.

Zaidi waweza kuangalia mwonekano wa simu ya Samsung Galaxy S8 na Galaxy S8 Plus hapa chini.

Share:

Leave a reply