VIDEO: Waziri Kigwangalla amaliza mgogoro wa ardhi uliodumu miaka minne

142
0
Share:
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amemaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka minne baina ya Hifadhi ya Msitu wa Utete maarufu kama Msitu wa Kale na vitongoji vinavyopakana na hifadhi hiyo vya Siasa, Nyawanje, Kindwitwi na Utunge katika wilaya ya Rufiji mkoani Pwani.
Dk. Kigwangalla amemaliza mgogoro tarehe 15 Februari, 2018 kwa kumuagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo kuunda timu ya wataalamu watakaoshirikiana na wataalamu wa mkoa wa Pwani na wilaya ya Rufiji kwa ajili ya kufanya tathmini ya eneo lenye mgogoro na kuanzisha mchakato wa kisheria wa kurekebisha mipaka ya eneo hilo na hatimaye kuligawa kwa wananchi.

Share:

Leave a reply