VIDEO: Waziri Mwakyembe awakingia kifua wasanii kwa BASATA

617
0
Share:

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amelitaka Baraza la Sanaa la Tanzania (BASATA) kuhakikisha kuwa inawahoji wasanii kabla ya kuzifungia nyimbo zao.

Mwakyembe alitoa agizo hilo baada ya kufanya mazungumzo na mwanamuziki Ney wa Mitego ofisini kwake mjini Dodoma.

Alisema serikali haina nia mbaya na Sanaa ya Tanzania lakini hakuna uhuru usio na mipaka hivyo hata kama wanatunga nyimbo wahakikishe wanatunga nyimbo ambazo hazitakuwa na viashiria ambavyo vinaweza kuleta athari kwa jamii ya Tanzania.

Share:

Leave a reply