Vifo vyaongezeka kwenye ajali ya mnara China hadi kufikia 74

433
0
Share:

Vifo vimeripotiwa kuongezeka huko nchini China kwenye mnara wa ujenzi wa mitambo ya umeme iliyotokea jana mashariki mwa china, chanzo cha habari kutoka serikalini kimeeleza.

Taarifa hiyo ya habari kutoka serikali imenukuliwa ikisema kwamba ajali hiyo mbaya haijapata kutokea kwa tarkribani miaka miwili iliyopita na kuua watu wengi kiasi hicho.

Watu wengine wawili wameripoti kuumia katika eneo la tukio kwenye kituo cha kuzalisha umeme ambapo ujenzi ulikuwa ukiendelea ambapo vifaa vya chuma, vyuma na aina ya mbao ngumu ziliwaangukia na kuwajeruhi vibaya, taarifa ya shirika la habari la Xinhua.

Sehemu ya kupoozea umeme ilitengeneza karibu na mji wa Fengcheng katika jimbo la Jiangxi ambapo vifaa kadhaa vya teknolojia vingi vilianguka na kujeruhi watu na baadhi ya vitu vya umeme vililipuka vibaya, amesema, mkuu wa usalama kazini, Bw Yuan.

Zaidi ya vikosi vya waokoaji 500 pamoja na wanajeshi, askari wa zimamoto na askari wa kawaida wa kusaidia wakati wa majanga walipelekwa eneo la tukio kuendelea kutoa msaada kwa waathirika.

Rais wa China, Xi Jinping aliwataka watu na viongozi wa serikali za mitaa kujifunza namna ya kupambana na matukio kama hayo ya kutisha ya majanga katika sehemu za minara, vituo vikubwa vya kuzalisha na kupoozea umeme unaozalishwa, amesema kwamba tume maalum ya kupambana na majanga itasaidia ili kupunguza madhara zaidi kwa jamii.

Share:

Leave a reply