“Vijana hawana maadili, hatutawaachia madaraka sasa”-Mwenyekiti wa TLP, Mrema

334
0
Share:

Aliyekuwa mgombea wa Ubunge Jimbo la Vunjo kwa tiketi ya chama cha TLP, ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho, Dkt.  Augustine Lyatonga  Mrema  leo Juni 14.2016 ameibuka tena mbele  ya waandishi wa Habari na kueleza mambo mbalimbali namna alivyofanyiwa vibaya ‘figisufigisu’ na wapinzani wenzake ambapo amesema kuwa kwa sasa suala hilo amemuachia Mungu kwani anaamini Rais wa sasa Dk. John Pombe Magufuli atampa nafasi nono hapo baadae.

Mrema amesema hayo ambapo muda mwingi alitumia kuwasema wapinzani wenzake hasa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA)  kwa hatua yao ya kutomtambua Rais  Dk. Mohammed Shein na Rais Magufuli  na hatua yao ya sasa ya kususia vikao vya bunge kwa lengo la kutomtaka Naibu Spika.

Akisoma taarifa yake ndefu, Mrema amesema kuwa, Sekretarieti ya chama hicho iliyokaa Juni 8 mwaka huu  na tathimini yao walibaini katika uchaguzi uliopita Mwenyekiti wao Mrema amefanyiwa hujuma mbalimbali zilizopelekea kushindwa uchaguzi na kushindwa kutetea kiti hicho.

Pia Sekretarieti imesikitishwa na  kitendo cha wapinzani kuele keza nguvu zote katika jimbo hilo ambalo alikuwa analishikiria na kuligombea kiasi cha kumuangusha Mrema.

Aidha, Mrema akijibu swali la mwandishi wa mtandao huu juu ya umri na hali yake ya kiafya kuwa ni wakati sasa wa kuwaachia vijana kuongoza Taifa. Mrema alijibu kuwa haondoki sasa hivi kwani vijana wengi hawana maadili hivyo yeye ataendelea kung’ang’ania mpaka wanyooke na kuwa maadili ndipo atawaachia.

“Wewe unataka tuwaachie nchi mafisadi? Vijana ndio wanafanya haya ushenzi na kuwafanyia watu unyama?. Mimi nitaondoka lakini mahesabu yangu ninayo, Lakini kama nitaondoka sasa hivi nani atawakemea vijana hawa?. Mfano sasa hivi huko Bungeni si munaona. Sisi tutakomaa mpaka vijana wawe na maadili ndio tutawaachia nchi” alieleza Mrema wakati wa kujibu swali la mwandishi wa mtandao huu.

DSC_7659

Aliyekuwa mgombea wa ubunge Jimbo la Vunjo kwa tiketi ya chama cha TLP, ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho, Dkt.  Augustine Lyatonga  Mrema (Wa pili kutoka kulia) akielezea waandishi wa Habari namna alivyofanyiwa hujuma katika uchaguzi uliomalizika mwaka jana kwa upinzani kumuondoa. Wengine kulia ni Katibu Mkuu wa TLP, Bi. Nancy Mrikaria. wengie kushoto ni Mwenyekiti wa Wanawake Bi. Ester Mkasi akifuatiwa na Naibu Katibu Mkuu, Bwana Richard Lymo.

maxresdefault

Aliyekuwa mgombea wa ubunge Jimbo la Vunjo kwa tiketi ya chama cha TLP, ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho, Dkt.  Augustine Lyatonga  Mrema akizungumza na waandishi wa Habari(Hawapo pichani) katika mkutano huo mapema leo Juni 14.2016.

Share:

Leave a reply