Vijana watakiwa kuacha kukaa vijiweni

191
0
Share:

VIijana nchini wametakiwa kuacha tabia ya kukaa vijiweni na kulalamikia tatizo la ukosefu wa ajira, badala yake watumie fursa zilizopo kwenye maeneo yao kujiajiri wenyewe kwenye sekta binafsi.

Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Singida Elias Tarimo, wakati akifungua mafunzo ya siku saba kwa vijana 180 juu ya teknolojia ya ufugaji wa kuku na nyuki, kilimo cha mboga-mboga, uzalishaji wa nishati mbadala na utengenezaji wa majiko banifu katika maeneo yao.

Tarimo alisema vijana wengi wanakaa vijiweni kupiga soga wakisubiri ajira rasmi za kuajiriwa na Serikali kwa kwenye makampuni ambazo ni chache mno.

“Vijana ni lazima sasa mbadilishe mfumo wa maisha na mtamabue kuwa ajiri haziko tu serikalini au kwenye makampuni mbalimbali.Fursa za ajiri zipo tele kwenye kilimo,ufugaji wa kuku au nyuki.Pia katika uzalishaji wa nishati mbadala ikiwemo majiko banifu”,alisema.

Aidha,aliwahimiza vijana kujiunga kwenye vikundi kwa madai kwamba kwa njia hiyo,watakuwa wamejijengea mazingiza ya kuweza kusaidiwa misaada mbali mbali pamoja na kukopesheka kwa urahisi na taasisi za kifedha.

Awali mkurugenzi mkuu wa shirika la SEMA,Ivo Manyaku,alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha vijana kujitambua na kutambua fursa mbalimbali ambazo zitawainua kiuchumi.

Hata hivyo vijana walioshiriki mafunzo hayo yaliyondaliwa na Shirika la SNV na kuendeshwa na SEMA –Singida, wanasema licha ya kupata ujuzi lakini tatizo kubwa ni Taasisi na Asasi mbalimbali za kifedha zinazojishughulisha na utoaji wa mikopo nchini, kuweka masharti magumu na riba kubwa.

Wamesema hali hiyo umewafanya vijana wengi wasiokuwa na nyumba au viwanja vya kuweka dhamana kushindwa kunufaika na mikopo hiyo ili kupata mitaji ya kuanzisha miradi ya kiuchumi.

Peter Mpaki alisema pia upo urasimu mkubwa kwenye baadhi ya taasisi zinazotoa mikopo jambo ambalo linawakatisha tamaa vijana.

Kulingana na takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, zaidi ya asilimia 60 ya Vijana 400,000 wenye uwezo wa kufanyakazi mkoani Singida wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa ajira.

Share:

Leave a reply