Vikundi shirikishi vyasaidia kupunguza uharifu mkoani Tabora

192
0
Share:

Imeelezwa kuwa kuwepo kwa  vikundi vya ulinzi shirikishi katika wilaya mbalimbali za mkoa wa Tabora kumesaidia kupunguza vitendo vya uharifu vilivyokuwa vikifanywa na baadhi ya watu wasiowadilifu mkoani humo.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Wilbroad Mutafungwa wakati akizungumza na uplandfm ofisini kwake.

Kamnada Mutafungwa amesema Jeshi la Polisi mkoani humo limekuwa likitoa  askari mmoja kwa kila mtaa ambao unakikundi cha ulinzi shirikishi ili kuimarisha doria katika mitaa hiyo .

Nae Mwenyekiti wa jeshi la Sungu sungu wa kijiji cha Mwanihalanga katika kata ya mbutu wilayani Igunga Amesema katika kijiji chao hupanga watu kumi kwa ajili kushiriki kwenye ulinzi shirikishi wakati wa usiku na asitaka hutozwa faini .

Nao baadhi ya wenyeviti  na wajumbe wa serikalinza  mitaa mbalimbali mkoani humo wamesema wao hushirikiana vizuri na askari wa Jeshi la Polisi katika kuimalisha doria kwenye mitaa yao na kuwaripoti watu wageni wasiowatambua ambao hufika katika  maeneo yao.

Kwa upande wake Asha Jacobo ambae aliwahi kuibiwa kutokana na kutokuwepo kwa ulinzi shirikishi katika mtaa wake anaeleza umuhimu wa ulinzi shirikishi katika jamii.

Jeshi la polisi mkoani Tabora kwa kutumia Polisi jamii bado linaendelea  kufanya kazi ya kudhibiti uhalifu huku wananchi na viongozi wa serikali za mitaa mkoani humo wakihimizwa kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi katika mitaa yao.

Na Mussa Mbeho, Tabora

Share:

Leave a reply