Waalimu 2, mwanafunzi 1 mbaroni kwa kuvujisha mitihani kidato cha sita

518
0
Share:

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa watatu wakiwemo waalimu wawili na mwananfunzi mmoja kwa kosa la kuvujisha mitihani ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari ya Chang’ombe, walilodaiwa kufanya Mei 5 mwaka huu shuleni hapo.

Kamishna wa Kanda hiyo, Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari Mei 10, 2017 ameeleza kuwa alipokea taarifa kutoka kwa Afisa wa Baraza la Mitihani Tanzania Aron Mweteni, kwamba katika shule ya Chang’ombe alimkuta Mwalimu Musa Elius akiingia darasani na mwanafunzi ambaye ni mtahiniwa aitwaye Ritha Mosha wakiwa na karatasi yenye maswali na majibu ya somo la Kemia Practical.   

“Baada ya kuwakamata na kuwatilia shaka, ufuatiliaji wa awali ulifanyika kupitia baraza la mitihani na kubainika kuwa swali hilo ni miongoni mwa maswali ya mitihani ya kidato cha sita unaofanyika mwaka huu,” amesema.

Kamanda Sirro amesema watuhumwa hao watatu akiwemo pia Mwalimu Innocent Mrutu mkazi wa Kibamba ambaye ni mtuhumiwa wa tatu, wanaendelea na mahojiano na upelelezi utakapokamilika watachukuliwa hatua za kisheria.

Na Regina Mkonde

Share:

Leave a reply