Waamuzi kutoka Uganda kuamua mchezo wa marudiamo wa Young Africans na Wacomoro

360
0
Share:

Mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Young Africans ya Tanzania na Ngaya ya Comoro hatua ya awali utachezeshwa na Waamuzi kutoka Uganda, kwa mujibu wa taarifa ya  Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), waamuzi hao ni Alex Muhabi Nsulumbi atakapuliza filimbi uwanjani.

Nsulumbi atasaidiwa na Ronald Kakenya na Lee Okello wakati Mwamuzi wa Akiba atakuwa Brian Nsubuga Miro huku Kamishna akitokea Afrika Kusini ambaye ni Monnyenyone Lucas Nhlapo.

Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kama ambavyo Young Africans walithibitisha CAF majuma mawili yaliyopita kabla ya terehe ya mchezo huo ambayo ni Februari 18, mwaka huu.

Wanajangwani hao mpaka sasa wapo kifua mbele baada ya mchezo wa awali kuibuka na ushindi wa bao 5-0 mchezo uliochezwa nchini Comoro.

 

Share:

Leave a reply