Waandishi wa habari wanufaika na mafunzo kutoka Action Aid Tanzania

220
0
Share:

Taasisi ya Action Aid imefanya mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari nchini kutoka vyombo vya habari mbalimbali ambapo walipata fursa ya kupata elimu ya haki za binadamu, elimu ya kodi na jinsi ya kuandika habari za uchunguzi.

Mafunzo hayo yaliongozwa na Andrew Mbega kutoka Action Aid ambaye alizungumzia Haki za Binadamu, Samwely Mkwatwa kutoka Action Aid alitoa elimu ya kodi na Mhariri Mtendaji wa gazeti la Jamhuri, Deodatus Balile ambaye alitoa elimu jinsi ya kuandika habari za uchunguzi.

MO Blog ilipata nafasi ya kuhudhuria mafunzo hayo na kukuandalia habari picha jinsi mafunzo hayo yalivyofanyika.

DSC_1528

Mkufunzi kutoka Action Aid, Andrew Mbega akitoa elimu ya Haki za Binadamu.

DSC_0180

DSC_1542

Afisa Kampeni wa Action Aid, Samwely Mkwatwa akitoa elimu kwa waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa kulipa kodi.

DSC_1535

DSC_1526

Kamara Dickson kutoka TYVA akichangia mada.

DSC_1533

Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo hayo.

DSC_1550

DSC_1554

Mhariri Mtendaji wa gazeti la Jamhuri, Deodatus Balile akitoa elimu kwa waandishi wa habari jinsi ya kuandika habari za uchunguzi.

DSC_0202 DSC_0190

DSC_1594

Andrew Mbega akiandika maazimio baada ya kutolewa elimu ya haki za binadamu, elimu ya kodi na jinsi ya kuandika habari za uchunguzi.

DSC_1597

Share:

Leave a reply