Wabunge wapewa tano kwa kuboresha muswada wa sheria hifadhi jamii

77
0
Share:

Chama cha ACT-Wazalendo kimeipongeza wabunge kwa kuboresha muswada wa Sheria ya Hifadhi ya Jamii baada ya kusikiliza maoni ya chama hicho.

Pongezi hizo zimetolewa leo jijini Dar es Salaam na Katibu wa Itikadi na Uenezi ACT, Ado Shaibu wakati akizungumza na wannahabari.

“Tunawapongeza wabunge kwa kuboresha muswada wa sheria ya Hifadhi ya Jamii baada ya kusikiliza maoni yetu,” amesema.

Aidha, amewataka wafanyakazi kuendelea kupambana ili kupata jawabu la kudumu na endelevu kuhusu suala la kujitoa kwenye mafao, huku akiahidi kwamba ACT itawapa ushirikiano utakao takiwa.

Share:

Leave a reply