Wachungaji sita watiwa mbaroni Rwanda

288
0
Share:

Wachungaji wapatao sita ambao makanisa yao ni miongoni mwa makanisa 700 yaliyofungiwa hivi karibuni nchini Rwanda, wamewekwa kizuizini na Polisi wa nchi hiyo.

Wachungaji hao wanatuhumiwa kufanya mikutano ya siri inayodaiwa kuwa na lengo la kukaidi uamuzi wa serikali.

Hatua hiyo imekuja kufuatia amri iliyotolewa na serikali ya Rwanda kwa Jeshi la Polisi ya kuwaweka kizuini wachungaji hao, ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu Rais Paul Kagame kutuhumu kwamba idadi kubwa ya makanisa nchini humo ni haramu.

Rwanda inadaiwa kuwa katika mkakati wa kujadili sheria mpya ambayo itahusika na mashirika yenye misingi ya Imani na dini yanayoendeshwa na wahubiri kwa ajili ya kuhakikisha viongozi wa kidini wanakuwa na shahda za elimu ya theolojia.

Share:

Leave a reply