Wafanyabiashara Singida wahimizwa kujenga utamaduni wa kuwarithisha shughuli hizo watoto wao

247
0
Share:

MENEJA mahusiano kitengo cha biashara makao makuu NMB benki, Reynold Tony, amewahimiza wafanyabiashara nchini, kujenga utamaduni wa kuwaandaa mapema watoto wao kurithi shughuli za biashara.

Tony amedai kwamba, kwa njia hiyo biashara husika itakuwa endelevu na kuendelea kunufaisha familia kiuchumi kwa muda mrefu zaidi.

Meneja huyo mahusiano, ametoa wito huo wakati akitoa mafunzo ya namna bora ya kufanya biashara zenye tija, kwa wanachama wa klabu ya wateja wa NMB Benki, tawi la Singida.

Alisema wafanyabiashara ni lazima watambue kuwa wakati wanaendelea kuzeeka, na biashara yake nayo inazeeka.

“Mfanyabiashara ukiishatambua ukweli huo, basi huna budi kuanza mapema kuandaa watoto wako kuja kurithi uendeshaji wa biashara yako kwa ufanisi zaidi ……….. ikiwezekana ipanuke zaidi”,amesisitiza.

Reynold Tony

Meneja mahusiano kitengo cha biashara makao makuu NMB benki, Reynold Tony, akitoa mafunzo yake ya juu ya namna bora ya kufanya biashara zenye tija.Tony amewataka wafanya biashara nchini, kuwandaa mapema watoto wao kurithi shughuli za biashara,ili ziwe endelevu na kuendela kuzisaidia familia husika kiuchumi kwa muda mrefu zaidi.

Akisisitiza zaidi, alisema uzoefu unaonyesha wazi kwamba mfanyabiashara asiye na utamaduni wa kurithisha watoto wake mapema shughuli za biashara, akishazeeka au Mungu akimchukua, hapo ndipo shughuli ya biashara yake nayo inafia hapo hapo.

Katika hatua nyingine, Tony amewataka wafanyabiashara wakiwemo wale wakubwa, wahakikishe wanakuwa na watu wa kuwasaidia, akiwemo muuzaji mahiri na mwaminifu.

Mohammed Mbaga

Mmoja wa wafanyabishara mwanachama wa klabu wa NMB tawi la Singida,Mohammed Mbaga, akishirika kwenye mada ya ufanyaji biashara bora.

“Pia ni lazima awe na mtunza stoo mwenye sifa na zaidi awe na mtunza mahesabu aliyebobea kwenye kazi hiyo na muadilifu, kikosi hicho kitasaidia  biashara iweze kupanuka zaidi na kuwa endelevu, biashara na hasa ile kubwa,ni lazima iwe na timu nzuri”, alisema  na kuongeza wafanyakazi”;

“Ni sawa na timu ya mpira wa miguu… beki kazi yake kuzuia mpira usiingie golini (upande wa biashara, pasiwepo na hasara), kuna mchezaji kazi yake ni kugawa mipira ili fowadi aweze kufunga goli, tofauti na hivyo biashara husika haiwezi kuwa endelevu”.

NMB Singida

Viongozi wa klabu ya wateja wa NMB tawi la Singida,wakifuatilia maendeleo ya mkutano mkuu wa mwaka,uliofanyika mjini Singida.

Statron Chilongola,

Meneja wa NMB kanda ya kati, Statron Chilongola, akitoa nasaha zake kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa klabu ya wateja wa NMB tawi la Singida.

NMB Singida

Baadhi ya wanachama wa klabu ya wateja wa NMB tawi la Singida waliohudhuria mkutano wao mkuu wa mwaka uliofanyika kwenye ukumbi mkubwa wa mikutano wa kanisa la romani katoliki mjini Singida.(Picha na Nathaniel Limu).

Share:

Leave a reply