Wafanyabiashara washikiliwa na Polisi kwa kutishia kuwaua waandishi wa habari

252
0
Share:

Jeshi la Polisi mkoa wa Singida ,linawashikilia wafanyabiashara wawili mapacha wenye asili ya kiarabu wa umri wa miaka 47 wakazi wa Mughanga mjini hapa, kwa tuhuma ya kutishia kuwauwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali mkoani hapa, kwa kutumia silaha aina ya bastola.

Pamoja na kuwashikilia, pia wanashikilia bunduki zao mbili aina ya rifle.

Watuhumiwa hao ni Hussein na Hassan Salehe, na kwamba pamoja na tishio hilo la kuwaua, pia wamedaiwa kumbaka binti wa mwandishi wa habari, ili waandishi hao waweze kuwaandika zaidi kwenye vyombo vya habari.

Akizungumza wa waandishi wa habari, SSP Mayala Towo, alisema kuwa watuhumiwa hao walitoa vitisho hivyo Novemba, 7 mwaka huu saa 3.00 asubuhi, kwenye ofisi ya klabu ya waandishi mkoa wa Singida iliyopo Msufini mjini hapa.

Alisema watuhumiwa hao walitoa vitisho mbele ya Cales Katemana wa radio Standard mjini Singida, na kumwagiza kuwa tishio hilo la kuwaua kwa maneno na kubaka familia za waandishi wa habari, linawahusu waandishi wa habari wote wa mjini hapa.

img_0843Kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida,SSP Mayala Towo,akitoa taarifa kuhusu kuwashikilia wafanyabiashara wawili mapacha kwa tuhuma ya kutishia kwa maneno  kuwaua waandishi wa habari ambao walitangaza taarifa zao za kukamatwa na Polisi kwa tuhuma ya kushambulia binti yao hadi mimba ya miezi sita kutoka. Pia kutangaza tuhuma nyingine ya kushikiliwa kwa kuvunja mlango na kisha kuiba mali. (Picha na Nathaniel Limu)

Towo alisema kuwa watuhumiwa walitoa vitisho hivyo, kwa madai kwamba waandishi wa habari, wametangaza taarifa za tuhuma zao za kumpiga mateke na ngumi mbele ya polisi binti yake, Leila Hussein.

“Mara baada ya habari zao kutolewa katika vyombo vya habari, Novemba, 6 mwaka huu saa nne asubuhi, watuhumiwa walienda ofisi za radio Standard na kulalamika ni kwa nini wamerusha taarifa za tuhuma zao. Baada ya hapo, walienda ofisi za Singpress, na kutoa onyo kali mbele ya Cales, kuwa kuanzia sasa mwandishi habari yoyote atakayerusha taarifa zao, atakiona cha mtema kuni,” alifafanua.

Towo alisema uchuguzi wa awali umebaini kuwa watuhumiwa hao waliingia ofisi ya Singpress kwa nia ovu kutishia, kuhofisha na kuvuruga amani. Pia watuhumiwa hawakuwa na mamlaka ya kuhoji utoaji wa habari zilizotolewa na waandishi wa habari.

Kaimu kamanda huyo alisema wanatarajia kushawishi mamlaka zinazohusika kwamba watuhumiwa wanyang’anyewe bunduki hizo kwa kukiuka sheria ya katazo la mmiliki kutishia kuua.

Alisema faili la kesi ya watuhumiwa lipo kwa mwanasheria wa serikali na likipitishwa, watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

Na Nathaniel Limu, Singida

Share:

Leave a reply